AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
RC Makonda amesema ujenzi wa Jengo hilo ulisimama tangu mwaka 2014 lakini kupitia uongozi thabiti wa Rais Dkt. John Magufuli aliona hilo changamoto hiyo na kuamua kutoa zaidi ya Shilingi Billion 2.1 kwaajili ya kukamilisha ujenzi huo ili kupunguza kero kwa wananchi.
Aidha RC Makonda amesema Jengo hilo litaanza kutumika mwezi January mwakani ambapo ndani yake litakuwa na uwezo wa kuchukuwa Vitanda 100 vya Mama na Mtoto na fedha ya kununua Vifaa tiba ipo tayari. Pamoja na hayo RC Makonda amesema mbali na ujenzi wa Jengo hilo Serikali inaendelea na ujenzi wa Hospital ya Wilaya Mabwepande na tayari yupo kwenye hatua za kujenga Kituo cha Afya Kawe na Bunju ambapo miradi yote ikikamilika itasaidia kumaliza Changamoto za Afya Wilaya ya Kinondoni.
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK