Tiwa Savage afunguka mahusiano yake na Wizkid

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii maarufu wa muziki nchini Nigeria, Tiwa Savage amefunguka kuwa kwasasa bado yupo single hajapata mwanaume wa kuishi naye tangu aachane na mumewe,  Tee Billz  mwaka 2016.



Akihojiwa jana asubuhi na kituo cha radio cha The Beat 99.9 cha Jijini Lagos, Nigeria. Tiwa Savage  amesema hajawahi kuwa kwenye mapenzi na mwanaume yeyote tangu aachane na mumewe na wanaume wote anaoonekana nao ni marafiki wa kibiashara tu.

Kuhusu tetesi za kuwa anatoka kimapenzi na Wizkid, Tiwa amesema kuwa ‘Mimi na Wizkid ni marafiki wa kibiashara tu”, Na akaendelea kujibu kuhusu mustakabali wa mahusiano yake mapya kwa sasa.

“Bado nipo single kwasasa na hakuna hata mwanaume anayenitafuta DM“, amefunguka mrembo Tiwa Savage na kukazia kuwa kwasasa yupo bize na kazi yake ya muziki.

SOMA ZAIDI KISA CHA TIWA SAVAGE KUACHANA NA MUMEWE MWAKA 2016.

Mwaka 2016 kwenye exclusive interview na Pulse TV, Tiwa alisimulia jinsi ambavyo mume wake alikuwa akimfanyia ikiwa pamoja na kumtelekeza kwa kutotaka kujua chochote pale alipolazwa hospitali nchini Jamaica alikoenda kufanya video na Busy Signal.

Anasema wakati anajiandaa kwenda kushoot, alianza kutoka damu nyingi ukeni kiasi cha kupoteza fahamu. Alimpigia simu na kumtumia ujumbe mumewe ikiwa pamoja na kumtumia picha akiwa hoi kitandani lakini hakujibiwa hadi anatoka hospitali.

Siku amerejea Nigeria na akiwa amelala usiku wa saa nane, simu ya mumewe iliita kwa namba iliyohifadhiwa kwa jina la biashara lakini alishangaa iweje kampuni impigie usiku huo. Anadai alichukua simu ya mumewe na kuanza kusoma ujumbe wa WhatsApp na ndipo alipogundua kuwa huyo alikuwa ni mwanamke na maongezi yao yalionesha kuwa walikutana hotelini na kufanya mapenzi. Kutokana na kitendo hicho aliondoka na kwenda kwa rafiki yake.

Anadai kuwa amekuwa akificha kwa muda mrefu kuhusu mume wake, lakini amedai tangu mtoto wao azaliwa, hajawahi kutumia hata senti kwaajili ya familia yao kwamba Tiwa ndiye kila kitu.

Amesimulia pia jinsi ambavyo mume wake amekuwa na tabia ya kumzunguka kwenye malipo ya show zake ambapo ametolea mfano wa harusi aliyotakiwa kwenda kutumbuiza London. Anasema alibaini kuwa mumewe alilipwa gharama zote lakini hadi anaenda kutumbuiza alimueleza kuwa hakuwa amelipwa. Kwakuwa alikuwa anafahamiana na miongoni mwa waandaji wa harusi hiyo alimuuliza na kujibiwa kuwa walikuwa wameshamlipa mume wake hela yote, miezi minne nyuma.

“Unamuibia mke wako, na yeye haoni kama ameniibia mimi, kwahiyo ilibidi nitumbuize kwenye harusi bure, kwasababu alikuwa ameshatapeli hela na sijui alizifanyia nini,” anasimulia.

Kwa upande mwingine staa huyo alieleza jinsi ambavyo mume wake alikuwa akiishia maisha ya zaidi ya kipato chake na hivyo wakati mwingine kumfanya ajikute kwenye madeni makubwa ambayo alilazimika kuyalipa.

Tiwa alisema jambo ambalo mume wake alizingua zaidi na ambalo limesababisha mgogoro wao ni pale alikopa naira milioni 45 ambazo ni sawa na shilingi milioni 495 za Kitanzania na kuchikichia. Kwa hali hiyo Tiwa alianza kuhofia usalama wake kwamba wanaomdai mumewe wangeweza hata kumdhuru ama kumteka yeye na mwanae kwasababu ya deni hilo.

Pia Tiwa amezungumzia jinsi ambavyo aligundua mume wake anatumia cocaine kitu ambacho kilimuumiza sana.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo alikanusha kwa msisitizo kuwa hajawahi kamwe kumsaliti mume wake na Don Jazzy, Dr Sid wala 2Face na kwamba yupo tayari hata kuwekewa kifaa cha kubaini kama anasema uongo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad