Zitto, Mwigulu Watifuana Mtandaoni...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mbunge wa Jimbo la Iramba, Dk. Mwigulu Nchemba (CCM) ameibuka na kumwambia Mbunge mwenzake wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) kuwa ni wakala wa wakoloni.

Dk. Mwigulu amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter akimjibu Mbunge Kabwe baada kuandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa Rais Magufuli na Mwigulu kama wangekuwa ndio Mwalimu Nyerere na Oscar Kambona (Waziri Mkuu wa zamani Tanzania) wangekataa kumng'oa mkoloni nchini kwa sababu amejenga reli, shule, hospitali pamoja na bandari.

"Yaani wewe ulivyo hivi sasa hata ungekuwepo miaka ya 60 ungekuwa wakala wa wakoloni wa enzi hizo kama ulivyo sasa," ameandika Mwigulu kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Dk. Mwigulu ameongeza kuwa Rais Magufuli anapaswa kuachwa na kwamba Mbunge huyo wa Kigoma Mjini anaonekana kuwa mwili wake uko Tanzania lakini moyo wake unatumikia kitu kingine kabisa ambacho sio Tanzania.

Zitto Kabwe ambaye kitaaluma ni mchumi amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rais Magufuli ambayo tangu imeingia madarakani imejikita kwenye ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa reli ya kisasa, ujenzi wa bwawa la kufua umeme mto Rufiji na ununuzi wa ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Zitto Kabwe ambaye ni Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, mara kadhaa amenukuliwa akidai kuwa hali ya uchumi imeonekana kuzorota kutokana na kile anachokidai kuwa maisha ya wananchi yamekuwa magumu ingawa serikali imekuwa inajinasibu kwa kuboresha miundombinu pekee na kushindwa kustawisha uchumi wa mtu mmoja mmoja.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwigulu, huyu mzamiaji hivi punde Uhakiki unaendelea na atapekenyuliwa Uvira na Ruvuvu sio mbali na kwa taarifa yetu huyu alinyamazishwa kwa kupewa na kupelekewa Ughaibuni Tofali la Zahabu ambalo itabidi Takukuru inalifanyia kazi na mgao waKigamboni pia.

    Huyu ni mpotoshaji aliekiukana ana kwao. Na mazingira anayajenga ya Asylum seeker in phases kama wale Wasaliti wengine waiopata Grade A.

    Isitshe huyu ni wa Mirembe au Hujui..?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nasikia haali yake ya Afya kichwani imezua Mjadala na kufanya Faili la maombi ya Asylu kuwa na ksi ndoo kama si kuupiliwa mbali likisaidiwa na mgonjwa kitandaani.

      Hiyo Tamu.

      Delete
  2. Huyu asihangaike nae Mwigulu, huyu mzamiaji haramu hivi punde Uhakiki unaendelea idara za Uhamiaji na Ninja yupo kazini na atapekenyuliwa Uvira na Ruvuvu sio mbali na kwa taarifa yetu huyu alinyamazishwa kwa kupewa na kupelekewa Ughaibuni Tofali la Zahabu ambalo itabidi Takukuru inalifanyia kazi na mgao wa Kigamboni pia.

    Huyu ni mpotoshaji aliekiukana ana kwao. Na mazingira anayajenga ya Asylum seeker in phases kama wale Wasaliti wengine waliopata Grade A.

    Isitoshe huyu ni wa Mirembe au Hujui..?

    ReplyDelete
  3. Huyu asihangaike nae Mwigulu, huyu mzamiaji haramu hivi punde Uhakiki unaendelea idara za Uhamiaji na Ninja yupo kazini na atapekenyuliwa Uvira na Ruvuvu sio mbali na kwa taarifa yetu huyu alinyamazishwa kwa kupewa na kupelekewa Ughaibuni Tofali la Zahabu ambalo itabidi Takukuru inalifanyia kazi na mgao wa Kigamboni pia.

    Huyu ni mpotoshaji aliekiukana ana kwao. Na mazingira anayajenga ya Asylum seeker in phases kama wale Wasaliti wengine waliopata Grade A.

    Isitoshe huyu ni wa Mirembe au Hujui..?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio maana anajipendekeza Bunge la kule Ughaibuni anajua akirudishwa kwao atasepea Ughaibuni kama Asylum sasa kapata mchongo kwa mgonjwa Madawa yamewazidi nguvu au vipi?

      Anajisumbua bule bule, malehemu S. Sitta alimbeba bila kujua hali yake halisi na Uhalisia wake. alichofaya ili kua Ubinadau na Utanzania kwa aliekuwa Hastahiki kufanyiwa mtoto wa Nyakabiga.

      Delete
  4. Mie naaulizaga, ikiwa huyu ndio anajiita huko twta na fezibuku kuwa kiongozi mkkuku wa Ei si ti wazalendo Je Maalim sefu hajapata viza kingianchini tita..?? na wazifa pia.

    ReplyDelete

Top Post Ad