11/08/2019

Hemedy PHD "Nimegawa Sana Mbegu zangu, Sasa Hivi Nimesitisha Nina Watoto 6 Kila Mmoja na Mama Yake"

"Niliamua tu kusitisha kugawa mbegu kwa sababu nina watoto wa kutosha, sasa hivi kwanza nahitaji kuwalea kwa hiyo hayo mambo mengine baadae, nina mwanamke wangu halafu tunapendana sana, naangalia zaidi maisha na natengeneza pesa" - Hemedy Phd.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva na Mwigizaji maarufu wa filamu nchini Hemedy PHD mwenye umri wa miaka 31, amesema kuwa ana watoto sita(6) kila mmoja na mama yake na mwenye umri mdogo kabisa ana miaka mitatu (5) na wamepishana miezi miwili miwili.

"Mtoto wangu mkubwa ana miaka mitano walifuata wote wanapishana miezi miwili miwili, sitaki drama kila mtu ana mama yake lakini all in all nawapenda sana watoto wangu na itakuja siku mambo yote wazi kama mnyama future " amesema Hemedy PHD

Aidha Hemedy PHD ameongeza kusema kuwa girlfriend wake wa sasa alikuwa na ujauzito wa mapacha lakini mambo hayakwenda vizuri na kuharibika. Kama angefanikiwa kupata mapacha hawo watoto angeongezeka na kuwa wa nane(8).

Hemedy PHD kwa sasa anasema hataki kuongeza mtoto mwingine ila anasaka pesa ili kuwatunza waliopo
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger