Jaji wa New York amesema Trump arudishe dola milioni mbili alizochukua

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Jaji wa jimbo la New York ameamuru Rais Donald Trump azirudishe dola milioni mbili alizozichukua kwa matumizi yanayotajwa na mahakama kuwa ni kinyume cha sheria.

Fedha hizo ni kutoka mfuko wa misaada wa 'Trump Foundation', ambapo inadaiwa kwamba alizichukua na kuzitumia katika kampeni zake kwenye uchaguzi wa mwaka 2016 uliomuingiza madarakani.

Uamuzi huu ni sehemu ya mashitaka yaliyowasilishwa na ofisi ya mwanasheria mkuu wa Jimbo la New York dhidi ya mfuko wa misaada wa 'Donald J Trump Foundation' akiwemo rais mwenyewe na watoto wake watatu Donald Junior, Ivanka na Eric.

Mahakama pia imeelekeza watoto wa rais Trump wanaosimamia uendeshaji wa mfuko huo kupatiwa mafunzo ya uongozi na kujua namna ya kufanya maamuzi ya matumizi ya fedha kwa misingi inayokubalika kisheria.

"Donald Trump Jr, Eric Trump na Ivanka Trump - ambao pia walikuwa wakurugenzi wa Trump Foundation - wanapaswa kupata mafunzo ya lazima kuhusu majukumu ya kuwa watendaji na wakurugenzi wa mifuko ya misaada", mwanasheria mkuu wa New York Letitia James alisema.

Kutokana na uamuzi huo wa mahakama, rais Trump ametakiwa kukiri waziwazi juu ya matumizi mabaya ya fedha za mfuko huo na kueleza kwamba wakati mwingine atazingatia masharti ya matumizi ya fedha za mfuko huo.

Familia ya Donald Trump: Wake na watoto
Kila unachohitaji kujua kuhusu uchaguzi Marekani
Asasi ya kujitolea ya Donald Trump ilifungwa mwaka 2018 baada ya waendesha mashtaka kumshutumu kuwa anafanya kazi kidogo kuliko fedha zinazotumika.

Inadaiwa kuwa taasisi hiyo ya bwana Trump na watoto wake watatu inapaswa kutohusisha siasa, mahakama imetoa uamuzi.

Vilevile suluhisho pekee la kesi hiyo ni kuwa lazima fedha hizo zilipwe na Trump mwenyewe.

"Trump anapaswa kulipa dola 2,000,000, kiasi ambacho kitaenda kwenye taasisi ya msaada kama bado ipo," aliandika jaji Saliann Scarpulla.

Bi.Saliann amesema kuwa fedha hizo zinapaswa kwenda kwenye mifuko ya misaada minane ambayo Trump hana uhusiano nayo.

"Malipo ya fedha hizo ndio suluhisho la mwisho la kesi hiyo," amesema mwendesha mashtaka.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Jordan Libowitz ni msemaji kundi maalumu linaloendesha kampeni wajibu wa jamii na maadili mjini Washington.

"Huu ni uamuzi mzuri sana, kiasi cha dola milioni mbili si fedha chache hata kwa mtu kama Donald Trump. Tungependa kuona uamuzi wa mahakama ukienda mbali zaidi hata kuweza kutoa zuio kwa yeye na wanawe kupigwa marufuku kujihusisha na mifuko hii ya kijamii''Jordan Libowitz ameeleza.

Bwana Trump na mwanasheria wake wanasema kuwa kesi hiyo ina njama za kisiasa na kukilaumu chama cha Democrats kutumia kila mbinu ili kumuondoa madarakani.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad