JPM Aapisha Mabalozi 5, Wizi Wabainika Ubalozi Ethiopia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


RAIS  John Magufuli leo  Jumamosi, Novemba 23, 2019 amewaapisha mabalozi watano katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Mabalozi hao ni:

1. Maj. Gen Anselm Shigongo Bahati kuwa balozi Misri.
2. Mohamed Abdallah Mtonga Abu Dhabi.
3. Jestas Abouk Nyamanga (Ubelgiji).
4. Ali Jabir Mwadini (Saud Arabia).
5. Dkt. Jilly Elibariki Maleko (Burundi).



Akizungumza baada ya uapisho huyo, Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema;


“Naomba nichukue nafasi hii kuwapongeza na kuwapa pole mabalozi walioteuliwa na kuapishwa leo. Mheshimiwa rais tumebaini kuwa katika Ubalozi wa Addis Ababa kuwa kuna ubadhirifu mkubwa ulifanyika katika ubalozi huo, na mpaka sasa muambata fedha yupo mikononi mwa PCCB Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa).



“Pamoja na ubadhirifu huo kufanyika,  cha ajabu CAG alikuwa anaupa hati safi Ubalozi wa Addis Abbaba.  Sasa pamoja na CAG , Serikali tutakuwa tunafanya ukaguzi wa kushtukiza mara kwa mara.”



Naye Rais Magufuli, katika maneno machache aliyoyatoa baada ya hotuba ya Waziri Kabudi, alisema:

“Najua mengi yameshasemwa, kwa kifupi napenda kuwapongeza mabalozi niliowaapisha leo, mkaiwakilishe nchi yetu vizuri na nawapongeza kwa kuwa ndiyo mabalozi wa kwanza kuapishwa hapa Ikulu ya Dodoma” amesema Rais Magufuli.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad