11/08/2019

Laini za simu Milioni 30 hazijasajiliwa kwa alama za vidole


Wakati Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ikisisitiza kuwa Desemba 31, mwaka huu ndio mwisho wa kusajili laini za simu kwa alama za vidole, imeelezwa kuwa zilizosajiliwa kwa mtindo huo ni milioni 12.783 sawa na asilimia 29.21.

Jana bungeni jijini Dodoma naibu Waziri wa Wizara hiyo, Atashanta Nditiye alisema zimebaki siku 53 kabla ya ukomo wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole huku Watanzania wakiendelea kulia na ugumu wa upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa.

Nditiye alitoa wito kwa Watanzania kuendelea kusajili laini zao kwani muda ukifika, laini zao hazitakuwa hewani kwa kuwa zitazimwa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger