Mama Kanumba Achekelea Mfalme Zumaridi Kufungiwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


BAADA ya hivi karibuni Serikali kusitisha ibada katika Kanisa la Mchungaji, Diana Bundala ‘Mfalme Zumaridi’ lililopo jijini Mwanza, mama wa aliyekuwa staa wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa ameeleza kufurahishwa mno na kitendo hicho.



Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda, mama Kanumba alisema aliumizwa mno kama mzazi baada ya mchungaji huyo kumwambia mwanaye Kanumba yuko sehemu fulani halafu alipofika sehemu hiyo, hakukuta chochote zaidi ya kumpa maneno ya kukiri uongo kwamba atangaze amemuona marehemu mtoto wake.

“Ninawapongeza viongozi wa Serikali kwa kumfungia Zumaridi kwa sababu najua kuna wengine wamepitia changamoto kama zangu za kujua kwamba wanakwenda kuwaona watoto au ndugu zao ambao wamefariki dunia, halafu wakifika hakuna chochote, kiukweli inauma sana,” alisema mama Kanumba.


Mama huyo aliongeza kuwa, kitendo cha kanisa hilo kumpinga Mungu, ndicho kilimuumiza mno na kushindwana na Zumaridi kwani alipewa masharti ya kuinama na kumsujudia mchungaji huyo.

“Nilishindwa kabisa kumsujudia, sikuweza kumpinga Mungu wangu, nina imani kabisa watu wengine wamepotea,” alisema mama Kanumba.

Kwa muda mrefu, kanisa hilo la mwanamke aliyejiita Mfalme Zumaridi limekuwa likilalamikiwa kupotosha misingi ya Dini ya Kikristo hivyo kufungiwa kwake kumeibua shangwe kwa watu wengi.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad