Martin Kadinda Atoa Sababu ya Kutokuwa Karibu na Wema

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Martin Kadinda, amesema sababu ya kutoonekana kuwa karibu na Wema Sepetu ni kutokana na kuwa bize na biashara zake na kujiepusha kwenye vyombo vya habari tofauti na awali.


Martin Kadinda amefunguka  hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuwepo na taarifa kuwa ule ukaribu wao wa mwanzo umepungua ambapo ameeleza,

"Hayo ni mawazo binafsi ukiangalia kwenye mitandao ya kijamii nipo na Wema Sepetu, Mimi mwenyewe kwangu nilikuwa naye ni kwamba nimeamua tu kumuweka Wema nyuma sio mbele kama ilivyokuwa kwa sababu mimi nina biashara natakiwa kuifanya na yeye anatakiwa aendeleze maisha yake" amesema Martin Kadinda.

Aidha Martin Kadinda ameendelea kusema "Nimejaribu kutofautisha urafiki na kazi kwa sababu zamani labda nilimpa asilimia 80 ya maisha yangu lakini sasa hivi nimeamua kufanya 50 kwa 50 ila sio kwamba kuna utofauti tupo sawa" ameongeza

Pia akizungumzia suala la Wema Sepetu kutojenga nyumba amesema, hayo ni mambo binafsi ya mtu hakuna aliye na ushahidi kama amejenga au hajajenga, kila mtu anakuwa na mipango au mawazo yake ya kufanya.




-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad