Ndemla atakiwa Singida UTD kwa mkopo.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kocha Mkuu wa Singida United Nsanzurwimo Ramadhani ameonyesha nia kumtaka kwa mkopo kiungo wa Simba Said Khamis Ndemla, ambaye amekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Tanzania bara.

Singida United imekuwa na wakati mgumu msimu huu kwani mpaka sasa  inaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi, ikiwa imejikusanyia alama nne tu.

Nsanzurwimo amesema wamedhamiria kuhakikisha wanaibakisha timu hiyo ligi kuu, hivyo watatumia usajili wa dirisha dogo kusajili nyota wenye uwezo.

Hata hivyo changamoto za kiuchumi zilizoikumba timu hiyo huenda zikawafanya washindwe kuipata huduma ya Ndemla, kutokana na masharti yaliyowekwa na Simba kwa timu zinazowataka wachezaji wake kwa mkopo.

Hivi karibuni Mtendaji wa Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa alisema timu yoyote inayomtaka mchezaji wa Simba kwa mkopo lazima ithibitishe kuwa na uwezo wa kumlipa mshahara wake anaolipwa Simba kwa muda wote atakaoichezea timu hiyo.

Alisisitiza Simba haitakuwa tayari kuingia gharama ya kulipa mishahara ya wachezaji ambao wanazichezea timu nyingine kwa mkopo.

Klabu ya KMC nayo inamuwania kwa mkopo winga Rashid Juma.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad