Yaliyojiri Kortini Kesi ya Alimchoma Mkewe kwa Magunia ya Moto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MAPEMA leo Jumatatu, Novemba 18, 2019, katika Mahakama ya Halimu Mkazi Kisutu kesi inayomkabili mfanyabiashara Hamis Luwongo (38) anayedaiwa kumuua kisha kumchoma moto mkewe, Naomi Marijani kwakutumia magunia mawili ya mkaa, upande wa jamhuri umeeleza kuwa jarada la kesi hiyo lipo katika hatu za mwisho la uchapaji.



Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon Mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Salum Ally amesema kuwa jarada lipo kwenye hatua ya mwisho ya uchapaji na baada ya hapo linatakiwa lipelekwe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria.



Kwa upande wake Wakili wa utetezi, Mohammed Majaliwa alisema hana pingamizi na ombi hilo, hivyo hakimu Salum Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 2 mwaka huu na mshtakiwa amerudishwa rumande.



Mshitakiwa anadaiwa Mei 15, 2019 katika eneo la Gezaulole Kigamboni Dar es Salaam alimuua mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad