Amenisomesha, Kaninunulia Gari Lakini Sina Mapenzi Naye! Nifanyeje?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Amenisomesha, Kaninunulia Gari Lakini Sina Mapenzi Naye! Nifanyeje?
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 Naishi Tabata jijini Dar nimejitokeza kwenu kuomba ushauri, Mimi na mpenzi wangu ambae amenisomesha toka form one hadi sasa nipo chuo kwani wazazi wangu walifariki wakati mimi nikiwa mtoto mdogo sana.

Sasa huyu mpenzi wangu amenigharamia sana yani kuanzia nguo zote hadi chakula nacho kula vyote ni msaada wake yeye na amejitolea kuninunulia gari la kutembelea na kanambia nitafute kiwanja ili tujenge nyumba ya kupangisha.

Ila mimi kwa sasa naona kama huyu mwanaume hatuendani kwani yeye hana elimu ila anafanya kazi kutumia akili ya kuzaliwa, Jamani mimi nataka kuishi na msomi mwenzangu ila huyu kaka mimi naona kama freemasson kwani kanisaidia sana asije akanitoa kafala, Mimi kwa sasa nimepata mpenzi mpya ambae anaelimu ya chuo pia ni sharo sio mshamba kama huyu wa zamani.

Sasa please naombeni ushauri wenu jamani nimwambiaje kama sipo tayari kuishi na yeye huyu mpenzi wa zamani bila kuumiza moyo wake...?

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Leo ndiyo umemuona mshamba na Free mason, wakati unakula, unavaa na kusoma tangu ukiwa huko form one mpaka leo hukuwaza kama atakutoa kafara, leo ndo unaona utatolewa kafara? acha kumtafutia sababu mtu wa watu, wakati unakubali hayo yote hukujua kama humpendi.
    Mimi siyo Free mason lakini ingekua mimi unanifanyia hivyo ningekukamua damu ukiwa hai niinywe yote, alafu nikukatekate nipike supu ninywe nile nyama yako mbwa koko usiye na shukrani wewe.

    ReplyDelete
  2. we msaliti tu MUNGU anakuona kwanini hukuviona toka hauna ata aibu


    ReplyDelete
    Replies
    1. Pamoja na elimu uliyoipata na kupendezeshwa na huyo mshamba mpaka ukapendwa na sharo bado unamuona free mason ama kweli kusoma si kuelewa unaweza ukawa na elimu lakini bado ukawa hujielewi, sasa muache huyo aliyekutoa tongotongo nenda kwa huyo unayemuona mjanja halafu uone mwisho wenu utakuwaje, paka la bar wewe huna hata haya kuandika hayo uliyoandika mwache mshamba wa watu nenda kwa huyo mjanja mle bata ila usithubuu kumchuna mshamba ukampelekea sharo, pamoja na ushamba wake atakuua we unajua hizo pesa alizokuhudumia tangu ukiwa mjinga mpaka hapo ulipofika unajua anapozitoa?

      Delete
  3. Jitahidi kuludisha mapenzi kwa huyo aliekusomesha.Kuludisha fadhila ni kitu cha msingi sana.
    Huyo sharo kakupenda kwasababu umesoma una gali sivinginevyo.Huyo jamaa kumwacha ukaambatana na huyo sharo wako ni sawa sawa na kumkana mama yako mzazi aliekuzaa akakulea mpaka ukawa mkubwa.

    ReplyDelete
  4. Huo ni Ulimbukuni ambao ni mwanzo wa kuharibikiwa katika maisha.. Masikini Nakuonea huruma

    ReplyDelete
  5. Just be with the one you really love.
    LOVE IS NOT POLITICS' Misaada, zawadi, kusomeshwa siyo justification ya kuumpenda mtu

    ReplyDelete

Top Post Ad