Chato Waanza Kutekeleza Agizo la Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Geita. Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita nchini Tanzania imeanza kutekeleza agizo la Rais wa nchi hiyo, John Magufuli alilolitoa la kutaka ujenzi wa upanuzi wa Hospitali ya wilaya hiyo kuanza mara moja.

Jana Ijumaa Desemba 6, 2019 akiwa hospitalini hapo Rais Magufuli aliwataka viongozi wa halmashauri hiyo kuacha kupoteza muda mwingi wakibishana juu ya upanuzi huo na kumtaka Waziri wa Tamisemi, Seleima Jaffo na  mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Eliud Mwaiteleke kuhakikisha ujenzi unafanyika kwa gharama zinazostahili.

Kufuatia agizo hilo, Mwaiteleke kwa kushirikiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Ligobeth Kalisa leo Jumamosi Desemba 7, 2019 wameanza kusimamia ujenzi wa hospitali hiyo unaotarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi minne.

Katika taarifa iliyotolewa na ofisa habari wa halmashauri hiyo, Richard Bagolele  imeeleza ujenzi wa upanuzi wa hospitali hiyo utahusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje, maabara, jengo la baba, mama na mtoto, jengo la wazazi pamoja na sehemu ya kuchomea taka ambayo yote kwa pamoja yatagharimu Sh1 bilioni.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad