Binti Analazimisha Ndoa Anataka Mpaka Kunisaidia Kutoa Mahari....

Awali ya yote nina mwanamke mmoja ambaye tulianza naye mapenzi toka tuanze wote kazi kwa sababu tumeajiliwa sehemu moja ila tu tunatofautiana sehemu ya kufanyia kazi yeye anafanyia wilayani na mimi nafanyia mkoani sasa toka tuanze imefika kipindi akabeba ujauzito na saizi ni miezi mitano tangu abebe huo ujauzito

Sasa anataka nikatoe mahali kwao ili wanitambue wazazi wake rasmi yeye ndio mpanga mahali na anasema ni milioni moja mahali pamoja na masufuria ya shangazi na babu na bracket la bibi mimi nikamwambia kuwa hicho kiasi sina akasema kuwa yeye atoe laki nne na mimi nimalizie laki sita na leo kanipigia simu kuwa inatakiwa ipelekwe barua ya kishika uchumba pamoja na elfu thelathini mimi nikasema kuwa saizi sina hela yeye akasema kuwa mimi niandike barua atakuja kuichukua na ataituma nyumbani kwao kwa njia ya posta na ataiweka hiyo elfu thelathini na kuituma nyumbani

Sasa ninacho jiuliza anataka tuoane mapema ili amiliki baadhi ya vitu vyangu pale tutakapo tofautiana tugawane au kwa sababu mpaka sasa nina nyumba tayari na magari kadhaa na nikikubali atoe siku tumegombana si ndio ataanza kutamba kuwa nilikutolea na mahali au anaharakisha ili aje tukae wote ili kakibanda kangu afanye kiburi ili tukauze jamani hebu tupeane mawazo na kiumri ananizidi yeye ana 28 na mimi nina 25

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments