Bunge Laanzisha Kwaya, imetumbuiza leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kwaya ya Bunge la jamuhuri ya muungao wa Tanzania,  kwa mara ya kwanza leo imeimba katika ufunguzi wa mkutano wa 18 kikao cha kwanza  cha bunge la 11 kilichoanza Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Jobu Ndugai ameipongeza kwaya hiyo ya bunge ambapo amesema leo imeimba vizuri wimbo wa Taifa na wa jumuiya ya Afrika mashariki wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.

Awali, wimbo wa Taifa na wa Afrika mashariki  kwenye ufunguzi wa mikutano ya Bunge ulikuwa unaimbwa na kwaya ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT) lakini leo umeimbwa na watumishi wa Bunge ambao walivaa majoho nadhifu ya mchanganyiko wa rangi nyeusi na blue.

Baada ya kumaliza kuimba na dua ya kuliombea Bunge na Taifa, Spika Ndugai alieleza kuwa hatua ya kwaya kuimba wimbo huo inatokana na uamuzi wa kamati ya uongozi ya Bunge uliotolewa Januari 2020.


Pia amelishukuru Jeshi la polisi Tanzania kwa kuwafundisha watumishi hao ambapo baada ya kuimba wabunge waliwapigia makofi na kuwapongeza.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad