Iran Yaitaja Wizara ya Ulinzi Marekani Kama Kundi la Kigaidi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



SHIRIKA la habari la Iran limesema, bunge la nchi hiyo leo limeitaja wizara ya ulinzi ya Marekani kuwa ni kundi la kigaidi.

 

Habari zinasema, kwa mujibu wa kura zilizopigwa na wabunge wa Iran, idara zote na kampuni zenye ushirika na wizara ya ulinzi ya Marekani, na makamanda wa Marekani waliopanga na kumuua aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Bw. Qassem Soleimani, wamewekwa kwenye orodha ya kundi la kigaidi.

 

Kadhalika, Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ameidhinisha kukiongeza Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Euro milioni 200.

 

Khamenei, jana usiku aliidhinisha kutolewa fedha hizo kutoka kwenye Hazina ya Maendeleo ya Taifa kwa ajili ya Kikosi cha Quds cha SEPAH.

 

Aidha katika kikao hicho cha leo, Wabunge wa Iran wamepitisha kwa kauli moja hoja ya ‘Kulipa Kisasi ‘ ambayo itaandaa mazingira kwa Iran kulipiza kisasi dhidi ya Marekani kwa kumuua Jenerali Qasem Soleimani, aliyekuwa Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad