1/14/2020

Kitu Gani Kimemkuta Vanessa Mdee?


By Sangu J

Moja ya mambo yananishangaza Sana kwenye Muziki wa Bongo Fleva ni kukosekana kwa Mwanamke mmoja ambaye atakuwa na hasira kubwa Sana kama aliyokuwa nayo Diamond Platnumz kwa kuweka rekodi ambayo hakuna Msanii aliyefikia.

Kiukweli Kwa Tanzania hakuna mziki mwepesi Sana kama mziki wa BongoFleva hasa kwa wanawake kuweka rekodi ambayo haijafikiwa na Msanii yeyote na ndiyo maana kila siku ni rahisi Sana akitokea Msanii mpya wa kike ni rahisi kuingia namba moja.

Mwaka 2016 niliandika makala moja ikimkosoa Lina Sanga namna anavyokimbizwa na Vannesa Mdee na nilimpongeza sana Vannesa kwa Hustle alizokuwa anazifanya na niliona matumaini makubwa sana kwa Vanessa lakini kwa nashangaa Vanessa na yeye sijui kakumbwa na jini gani.

2016 game ya wasanii wakike ilikua inaongozwa na Vanessa na tuliona mafanikio mengi sana kwake alishiriki project nyingi sana za nje

 nakumbuka alishawahi kumkabidhi tuzo ya mtumbuizaji Bora ya MTV - MAMA Diamond Platnumz Mwaka 2015

 kiukweli niliamini Music wa Bongo Fleva Kwa upande wa wawanake sasa ulishaanza kupaa kwa kuwa tulikuwa na Vanessa Mdee.

Cha kushangaza leo 2020 miaka 4 baada ya kumsifia sana Vanessa na kwenye andiko langu la nasikitika leo kuandika tena nikiyakataa maneno yangu ya 2016 kwa kuangushwa tena na Vanessa yaani Vanessa amekuwa msanii sio wa majaabu tena vitu vikubwa vinapita lakini hatuoni ushiriki wake kama miaka kadhaa nyuma itakuwa ameshachoka anapigwa vita sana au ndiyo ule usemi kwamba wasanii wa kike hawapendani ndiyo imemrudisha nyuma yeye.

Kiukweli Vanessa amewakatisha tamaa ambao tulimwekea Imani kubwa sana kwa watu kwa sababu naona nafasi yake inaenda kuchukuliwa na Nandi kwa mapambano anayoyafanya naamini kama hatokata tamaa mapema nadhani atafika mbali zaidi.

Ukiniamhia 2019 Vanessa kafanya nini sikumbuki kwa sababu zaidi ya skendo za kuachana na kupata mpenzi mpya kitu ambacho hatukukizoea kwa Vmoney na nadhani anguko lilianzia pale alipotengeneza kiki na Shilole ili muharibia sana kisanaa nadhani Vanessa anapaswa kujiangalia wapi aliteleza kwa 2019 ukitoa EAGT nadhani tulitarajia makubwa zaidi kama tour za kutosha, show za nje kama zote, muendelezo wa show zako.

Naamini Vanessa 2020 atakua amejipanga vya kutosha ili kumrudisha Vanessa wa miaka 3 nyuma.

Toleo lijalo nitaandika kwa jinsi gani Nandi anaenda kuwa namba 1 kwa muziki wa wanawake 2020 hadi 2021.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger