Polisi Wamkamata Akisafirisha Vipodozi Haramu Akijifanya ni Mtoto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanamke mmoja aliyekuwa akivuka mpaka wa nchini Uganda kutokea nchini Congo, amekamatwa na maafisa wa polisi akiwa amebeba vipodozi haramu alivyokuwa amevifungasha na kuvivalisha kwenye nguo ya mtoto, ambayo ilileta uhalisia wa mtoto mdogo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Bidhaa nchini Uganda, Dickson Kateshumbwa, amesema kuwa bidhaa hizo zilikuwa zimepakiwa vyema katika nguo za mtoto ili kuonekana kwamba ni mtoto, huku Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA), ikisema kuwa tayari imekwishaitambua mbinu hiyo, hivyo si rahisi kwa msafirishaji yeyote wa vipodozi bandia kupita salama nchini humo.

"Mtoto ghushi alipandishwa gari la kutoka Congo katika kituo cha mpaka wa Mpondwe, na baadae iligundulika mtoto huyo kuwa ni mwanasesere aliyekuwa amesakamiwa vipodozi haramu, baadhi ya walanguzi huendelea kushangaza" alisema Kateshumbwa.

Serikali ya Uganda ilipiga marufuku vipodozi hivyo tangu mwaka 2016, kwa sababu ya kuwa na viwango vya madini ya zebaki na hydroquinone, ambapo utafiti kadhaa umefichua kuwa vina madhara kwa afya, ambapo pia Idara ya Ubora wa Bidhaa (KEBS), iliorodhesha baadhi ya mafuta na bidhaa za urembo ambazo zilikosa, kutimiza masharti ya ubora mnamo Novemba 2019.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad