Waziri Mwakyembe "Wanaotaka SAMATTA ajengewe sanamu Tulieni Kwanza Alipofika Sio Kilele Cha Mafanikio"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe amewataka Watanzania kumuombea Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta, ili aweze kufanikiwa katika klabu yake mpya ya Aston Villa ambayo amesaini mkataba wa miaka 4 na nusu.


Waziri Mwakyembe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV na EA Radio Digital ili kupata kauli ya Serikali kuhusiana na hatua aliyofikia Mbwana Samatta.

Mwakyembe amesema kuwa "hakika kama Serikali tumefurahi kama walivyofurahi Watanzania wote, tunampongeza sana Samatta kwa juhudi zake najua hakubahatisha, ila kwa nidhamu ya hali ya juu, na hiki ndiyo kinawakwamisha vijana wengi wa Kitanzania mtu akikupa safari mbili unajiona umemaliza." - Waziri Mwakyembe

"Wanaotaka SAMATTA ajengewe sanamu, wasikimbilie masuala ya sanamu, tumuombee afanye vizuri kwanza, hata tukijenga sanamu lakini asipofanya vizuri Aston Villa haitaleta maana, alipofika Samatta sio kilele cha mafanikio tunataka awe Messi wa Dunia nyingine" - Waziri Mwakyembe
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad