"Weka akiba ya maneno, leo mimi kesho inaweza kuwa wewe' Stamina amvaa Mc Pilipili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii wa bongo fleva Stamina ambaye anatamba na kibao chake kipya 'Asiwaze' kilichokuwa gumzo midomoni mwa watu amemjia juu Mc Pilipili baada ya kumkejeli na kumtaka aweke akiba ya maneno kwani yanaweza kumkumba kama yaliyomkumba kwenye ndoa yake.

Mc Pilipili alimsema Stamina kuwa asiwahusishe kwenye matatizo yake binafsi kwakuwa yeye amelipa milioni 8 kwa mkewe awezi kuichukia ndoa lakini leo kupitia instagram Stamina amemjibu hivi Mc Pilipili;

''Matatizo na Changamoto Ndani Ya Ndoa Yanaweza Kumkuta Mtu Yoyote Yule, Leo Ni Mimi Lakini Kesho Unaweza Ukawa Ni Wewe, Usijione Uko Salama Sana Ndani Ya Ndoa Yako Kaka (Weka Akiba Ya Maneno, Punguza Kejeli Na Dharau Utaheshimika Na Kupendwa Zaidi)
Usiharibu Na Kupoteza Sifa Na Heshima Uliyokuwa Nayo Kwa Kuzipaka Matope Ndoa Zingine Na Kuona Wewe Pekee Ndio Mwenye Ndoa Iliyo Imara!! Ipo Siku Utazipaka Matope Ndoa Na Harusi Unazozisimamia Kama MC Na Zitaharibu Biashara Yako Na Career Kwa Ujumla!! Unaongea Kwa Kujiamini Sana Kwamba Ndoa Yako Iko Salama Na Haiwezi Kuyumba, Na Unatuona Kama Sisi Wengine Hatuijui Ndoa Ila Ndoa Yako Tu Ndio Pekee iliyobarikiwa, Watu Wamekusikia Na Watatunza Maneno Yako Kama KumbuKumbu Na Muda Ndio Utaongea.

MALIPO NI HAPAHAPA DUNIANI!!
Ubarikiwe Sana na kila la kheri katika ndoa yako🙏''

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad