Zijue Athari za Kuoa Mwanamke Mzuri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



AWALI ya yote naomba niseme kwamba, raha ya ndoa ni kumpata mtu ambaye anajua maisha na anajua mapenzi pia. Ukipata mwanamke ambaye anajua kutafuta pesa tu lakini kwenye ulimwengu wa mapenzi ni limbukeni, atakusumbua sana.

Lakini pia ukijichanganya ukaoa mwanamke ambaye ni mtaalam wa mapenzi lakini hajui pesa inavyotafutwa, nalo ni tatizo licha ya kwamba kwa wengine si tatizo kwani wapo ambao hawataki kuoa wanawake wenye vipato kutokana na yale yanayosemwa kuwa, baadhi yao wakijua kutafuta pesa, wanakuwa viburi.

Hata hivyo, kwa wanaume wanapofikia muda wa kuoa kila mmoja huwa na chaguo lake. Kila mtu atakuwa na vigezo vyake ambavyo vinaweza kutofautiana kutoka kwa mmoja hadi kwa mwingine.

Tofauti hiyo inakuja hata kwenye suala la tabia na uzuri. Kwa mfano, wapo ambao wanaangalia sana suala la tabia nzuri na muonekano mzuri pia. Lakini unaweza kushangaa mwanaume akatafuta mwanamke ambaye anakunywa pombe na anayependa kujirusha kwa kuwa na yeye ni mtu wa mambo hayo.

Aidha, wanaume wengine watakuambia hawataki kuoa wanawake wanaokunywa pombe, wanaoendekeza mambo ya anasa. Wanataka wanawake wa kutulia nyumbani, wanaomjua Mungu. Huo ni utofauti mdogo tu kwa baadhi ya wanaume wanapochagua wanawake wa kuingia nao kwenye ndoa.

Hata hivyo, hili suala la kutaka kuoa mwanamke mzuri huwa lina tofauti ya aina yake. Mwanamke ambaye wewe unaweza kuona ‘umeng’oa kifaa’ wenzako wanaweza kukuponda kwa kusema umependa demu asiye na hadhi yako. Ukweli uko hivyo kwamba, kibaya kwako ni kizuri kwa mwenzio.

Nigeukie sasa kwenye kile nilichodhamiria kukizungumzia leo. Ni kuhusu athari ambazo mwanaume anaweza kuzipata endapo ataoa mwanamke mzuri kwa sura na umbo, mwenye pesa lakini limbukeni. Hapa namaanisha kwamba, wapo ambao ni wazuri, waliokwenda shule, wenye kazi zao ila wanapoingia kwenye maisha ya ndoa, wanawaheshimu waume zao kupita maelezo. Yaani vipato vyao, elimu na mali zao havina thamani mbele ya mume.

Ukibahatika kuoa mwanamke wa sampuli hii utayafurahia maisha. Lakini ukioa aliyejaaliwa vitu hivyo kisha akawa si muelewa wala hajui thamani ya mume na ndoa, andika maumivu. Kimsingi zipo athari nyingi za kuoa mwanamke mwenye pesa, mzuri kwa muonekano, ‘aliyebukua’ sana lakini akawa limbukeni. Leo nitagusia tatu.

Kusalitiwa kuko nje nje

Uchunguzi unaonesha kuwa, wanawake wengi malimbukeni ambao wanajijua ni wazuri na wana pesa zao wakiudhiwa kidogo tu ni wepesi kuchepuka hata kwa kuwashawishi wanaume wengine kwa pesa. Utakuta mume kamkosea kidogo au kamkera bila kudhamiria lakini yeye anaona njia sahihi ni kutorudi nyumbani. Anaweza kwenda kulala hotelini mpaka pale mume atakapomfuata na kumpigia magoti. Wapo wanawake wa hivyo!

Ni wepesi kuomba muachane

Ukifuatilia sana wanawake wenye vigezo hivyo wanajiamini sana, hawa ndiyo wanaoongoza kwa kuomba talaka. Kosa dogo tu, atakuambia kama vipi muachane.

Anasema hivyo akijua wapo wanaume wengi wanaomsumbua na hatapungikiwa lolote. Tena hali inaweza kuwa mbaya sana kama wakati huo hamjajaaliwa mtoto kwani atajua hatakosa kitu akikuacha. Pesa anayo, ana uhakika wa kupata mwanaume mwingine fasta, kwa hiyo anaona hana cha kupoteza au kukikosa akikutosa.

Rahisi kukutawala

Chunguza sana utabaini kuwa, wanaume ambao wanasumbuliwa na wake zao wana vigezo hivyo. Baadhi ya wanawake wenye pesa na wanajijua ni wazuri wanapenda sana kuonekana wao ndiyo wenye sauti ndani ya nyumba. Watakataa kuelekezwa wala kupewa amri na wanaume zao hata kwenye masuala ya msingi. Hawa ndiyo wale ambao wanataka kurudi nyumbani muda wowote wanaotaka na wasiulizwe.

Watataka wawe wenye maamuzi ya mwisho na kila jambo la kifamilia washirikishwe laa sivyo kinanuka. Hili ni tatizo! Kimsingi ninachotaka kukifikisha kwa wanawake ni kwamba, ndoa ni heshima. Ukijaaliwa kupata mwanaume wa kukuingiza ndani, jitahidi kuithamini ndoa yako. Jua wapo wanawake wenye kila kitu lakini wamekosa wanaume wa kuwaoa na wanaitamani heshima ya ndoa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad