Jinsi ishara, Maajabu na Miujiza inavyotajirisha Wachungaji na Maustadhi feki.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Watu wamekuwa wahanga wa kubwa wa kutajirisha hawa wachungaji na maustadhi kwa kuendeshwa na imani ya ishara, maajabu na miujiza,

Wahanga hawa kwa asilimia kubwa mno wamekuwa ni wanawake ambao wameumbwa kudanganyika kirahisi mno.

Wachungaji na maustadhi feki wamegeuka kuonekana ni miungu mtu wakati kiukweli inabidi wawe wanahubiri neno la mungu,

Hali hii imepelekea mpaka kutengeneza matukio ya kuteka imani za wahanga na wengi tumeshuhudia haya matukio, kwa mwaka Jana pekee kuna mtu huko iringa aliyejinadi ni mchungaji alitengeneza tukio la kumnasa mchawi juu ya kaa lake ila ikaja kuthibitika baadae kwamba huyo aliejifanya ni mchawi walikubaliana na mchungaji feki watengeneze hilo tukio ili mchungaji apate ng'ombe(waumini) wengi na kisha kuwakamua maziwa(pesa).

Vivyo hivyo nao ma ustadh hawapo mbali sana maana kuna baadhi wanalipa matangazo kwa mastaa wa Instagram wawatangazie biashara yao ya kusoma visomo watu wenye mikosi, nuksi, n.k matangazo yao huwa yanga video ya mtu kugalagala kwa kile kinachidhaniwa wanatoa majini.

Wahanga wa hii miujiza ama kwa jina maarufu NG'OMBE" wamekuwa wakikamuliwa bila Huruma kitu kinachowafanya wachungaji na hawa maustaz kuwa mabilionea.

Kwa Leo naskia huko moshi watu 20 wamekufa kwa haya haya mambo, biashara zimekuwa nyingi za kujitajirisha kupitia hawa ng'ombe, kuna mchungaji kawakamata kisawasawa hawa ngombe mkoa flani kaweka vifurushi vya maombi, sikumbuki kiasi sahihi ila Kifurushi cha kifungua njia kilikuwa laki 5, kufungua mlango milioni 1 na kufungua geti ni milioni na nusu.

Cha ajabu hawa wahubiri wamekuwa wakiishi maisha ya juu na ya anasa ila hutokuja kusikia wakisaidia waumini wao hata ada za kupeleka watoto wao kusoma.

Mwenye macho na aone!!! Tumeshuhudia hawahawa wakamuaji wakiwa ni vinara wa ulevi waziwazi na wengine hata video zao kuvuja wakifanya uzinzi na waumini wao, mwenye macho haambiwi anaona!!!

Kama ulichofata kanisani ni miujiza nakushauri iende tu kwa waganga, wapo wengi
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad