Kweli Pogba siyo wa mchezo mchezo, Juventus wapo tayari kuwatoa sadaka Washambuliaji wake wawili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Katika hali isiyo ya kawaida unaweza usiamini lakini hapa ndipo unapoweza kuona ukubwa na umuhimu wa mchezaji, hasa linapokuja swala la usajili wake. Miamba ya soka ya Serie A, klabu ya Juventus inapanga kuwatoa Washambuliaji, Aaron Ramsey,mwenye umri wa miaka 29, na  Adrien Rabiot kijana wa miaka 24, kwa Manchester United kama sehemu ya kitita cha paundi milioni 125 ili kujaribu kumrejesha mchezaji wa Kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba 26. (La Gazzetta dello Sport, via Mail on Sunday)

Image result for Juventus 'planning £125m package to sign Manchester United star Paul Pogba and are considering offering Adrien Rabiot and Aaron Ramsey as part of the deal' as agent Mino Raiola 'makes contact with Italian giants'

Wakala  wa Pogba, Mino Raiola, amesema kwamba alifanya mazungumzo na Juventus kuhusu mchezaji huyo na kuna uwezekano wa kuondoka Manchester United msimu ujao. (Sunday Telegraph)

Wachezaji wa Manchester City waliitwa katika mkutano na mkuu wa klabu hiyo Ferran Soriano Jumamosi, saa moja baada ya timu hiyo kupigwa marufuku ya kushiriki kombe la ligi ya mabingwa kwa misimu miwili.(Sunday Telegraph)Mauricio Pochettino

Mauricio Pochettino aliiongoza Tottenham hadi fainali katika ligi ya Champions 2019
Aliyekuwa kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino anaweza kuchukuwa nafasi ya kocha wa Manchester City, Pep Guardiola iwapo raia huyo wa Uhispania ataamua kuondoka klabu hiyo. (Sun on Sunday)

Tottenham ingekuwa imemsajili wa Uingereza mshambuliaji Jack Grealish, 24, kwa £6m miezi 18 iliyopita lakini mwenyekiti Daniel Levy alikata kufikia makubaliano hao. (Sun)

Hatma ya maneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer iko mashakani baada ya kushindwa kuwasajili wachezaji watatu waliokuwa walengwa katika kipindi cha usajili cha Januari. (Star Sunday)Arsenal striker Pierre-Emerick Aubameyang

Aubameyang huenda akasajiliwa na Inter Milan
Meneja wa Inter Milan Antonio Conte ameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30. (Sunday Mirror)

Inter Milan itamruhusu mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 22, kujiunga na Barcelona iwapo itafanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 28. (Tuttosport, via Sunday Express)

Liverpool ipo katika mazungumzo ya mwisho mwisho a kumsajili RB Leipzigstriker Timo Werner, ikiwa na nia ya kufikia kiasi cha £48m kwa mchezaji huyo wa Ujerumani (Nicolo Schira, via Sunday Express)

Mchezaji wa Arsenal Kieran Tierney analengwa na meneja wa Leicester City Brendan Rodgers, ambaye aliwahi kuwa na mchezaji huyo wa Scotland, 22, wakati akiwa Celtic. (90min)
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad