TANZIA: Staa wa Filamu ya Queen of Katwe, Nikita Pearl Waligwa Afariki Dunia Akiwa na Miaka 15

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Muigizaji wa kike, Nikita Pearl Waligwa aliyekuwa mmoja wa wahusika katika filamu ya Queen of Katwe, iliyoangazia mtu mwerevu kutoka maeneo ya makazi duni ya Uganda, mcheza chess, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 15, kulingana na chombo cha habari cha Uganda.

Nikita Pearl Waligwa
Nikita Pearl Waligwa alikuwa amepatikana na uvimbe kwenye ubongo.

Katika filamu ya Queen of Katwe, iliyotoka 2016, iliakisi simulizi ya kweli ya Phiona Mutesi, ambaye alianza kucheza chess akiwa na umri wa miaka 9 licha ya kwamba hakuwa anasoma na akashiriki mashindano hadi kufikia kiwango cha Kimataifa.

Katika filamu hiyo Lupita Nyong’o aliigiza kama mama yake, huku David Oyelowo akiwa mwalimu wake wa mchezo wa chess.

Waligwa aliiigiza kama Gloria, rafiki ya Phiona ambaye alimuelezea sheria za mchezo wa chess.

2016, alipatikana na uvimbe kwenye ubongo na Mira Nair mwelekezi wa filamu ya Queen of Katwe, inasemekana kwamba alitafuta watu kuchangisha pesa ili kumsaidia katika matibabu ambayo alipangiwa kupata India, huku daktari wa Uganda akinukuliwa kusema kwamba hawakuwa na vifaa stahiki kwa matibabu yake.

Inasemekana kwamba mwaka 2017 alikuwa anaendelea vizuri lakini mwaka jana akapatikana na uvimbe mwingine.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad