Muongoza Filamu Maarufu na Tajiri Hollywood Hali Tete Kwa Ubakaji na Unyanyasaji wa Ngono..Yupo Pia Lupita Nyong'o Kwenye List

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Fahamu: Licha ya kuwa tajiri pichani Harvey Weinstein producer maarufu Hollywood amekanwa na watoto wake wakubwa watatu hawamtaki tena kuwa baba yao wamekata nae mawasiliano kabisa. -

Ni siku kadhaa baada ya Mahakama nchini Marekani kumkuta na hatia mzazi wao huyo kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono na ubakaji wanawake mbalimbali wakiwemo wasanii maarufu wa kike Marekani hasa mastaa wa filamu. Watoto wake hao waliomkana wote ni wa kike Lily(25), Emma(22) na Ruth(17) kutoka ndoa yake ya kwanza -

Harvey pia aliachwa na mkewe wa pili baada ya mwaka 2017 utiriri wa wanawake kujitokeza kila mmoja kwa Wakati wake kueleza kunyanyaswa kingono na wengine kubakwa na producer huyo aliyekuwa mwenye nguvu Hollywood kabla ya soo hilo

Harvey ametajwa kutumia nguvu yake ya pesa vibaya kunyanyasa wanawake kingono hasa wengi waliokuwa na umri mdogo na chipukizi Hollywood akiwaahidi deals mbalimbali. Miongoni mwa mastaa maarufu waliojitokeza kunyanyswa kingono ni pamoja na Angelina Jolie, Gweneth Paltrow, Lupita Nyong'o etc

Mkewe wa pili amesema alishtushwa sana, na kumwaga machozi Wakati akihojiwa na Vogue ambapo aliwapa pole wanawake na wasichana wote walionyanyaswa na mumewe kwa maumivu waliyopitia. Mkewe huyo wa pili licha ya kuzaa nae watoto wawili wenye miaka 9 na 6 , na yeye pia alimuacha mumewe huyo hivyo ndoa kuvunjika ili kuwapa sapoti wanawake husika ambapo ndio #MeTooMovement ikashika kasi -

Harvey anakabiliwa na miaka si chini ya 25 jela ambapo hukumu itatolewa tarehe 11 March
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad