3/31/2020

Aliyefariki kwa Ugonjwa wa Corona Kuzikwa Leo na Serikali ni Mdogo wa Bregedia Generali Mbita


Familia ya Marehemu Alhaj Brigedia Generali Hashim Mbita kwa huzuni kubwa inasikitika kutangaza msiba wa mdogo wao mpendwa Iddi Hashim Mbita aliyefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Mloganzila kwa ugonjwa wa Corona.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia hiyo imeeleza kuwa serikali itamzika leo mchana.

“Kutokana na tatizo lililopelekea kifo chake Corona serikali itamzika mpendwa wetu leo mchana. Wawakilishi wachache sana wa familia wataruhusiwa kuhudhuria mazishi,” taarifa hiyo imeeleza


Aliyefariki kwa Corona Iddi Hashim Mbita
Taarifa hiyo imeeleza kuwa hakutakuwa na msiba wala matanga ya pamoja kuepuka kueneza maambukizi.

“Kila mtu aomboleze kwake.
Dua nyingi tumuombee Iddi Allah amuweke pema peponi. Amina,” taarifa hiyo imeeleza.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger