3/27/2020

House Girl Kufua Boxer Zangu ni Sawa Kweli?

Kwa muda mrefu nimekua nikijiuliza swali hili kutokana na utaratibu uliopo nyumbani kwangu. Juzi nilikuta kuna ugomvi kati ya wife na house maid wetu, ambapo yule binti alikua amefura kwa hasira, kasimama katika mlango wa Chumba chetu akidai apewe pesa zake asepe usiku huo huo na alikua tayari ana begi mkononi.

Nikambembeleza, nikamuomba asiondoke usiku huo asubiri asubuhi, wife akatoka chumbani kama mbogo na kunigeuzia kibao kwamba kwanini nambeleleza kwamba nimwache aende na hapati hata senti, ukawa ugomvi mkubwa sana, ambapo binti kwa hasira akamjibu wife kuwa "" kama wewe ni mke bora usingeshindwa kumfulia mmeo hata boxer hadi unaleta kwangu, hufai""" kwa kweli sikuwahi kujua huwa anampa maid afue boxer zangu.

Huwa naona zimeshafuliwa na kupigwa pasi mimi navaa tu, juzi ndio niligundua hili suala, anyway yule binti alingangania kuondoka usiku ule kwamba yeye ni mtu mzima anajua anakoenda, tukaenda kwa Mjumbe nikampa nusu ya pesa anazodai zingine atarudia kama laki tatu hivi, kumbe siku zote nikitoa mshahara wife hampi anadai anamtunzia kwamba ataharibikiwa akimpa monthly.

Jana nikawa namuuliza wife kuwa kumbe boxer pia huwa unampa afue? Badala ya kunijibu kajikasirisha uongo na kweli ili tuiache hiyo mada, kwamba inakuaje nina mtetea housegirl hadi kufikia hatua kumbembeleza asiondoke, anyway hayo yakaisha.

Ila tu nikajiuliza swali hivi ni jambo la kawaida kwa maid kufua boxer zangu? Mimi ndio sielewi inavyokua maana wakati mwingine pale mbele ya boxer huwa panatengeneza miduara ya mabaki ya mbegu mara baada ya tendo usiku, yale matone huwa yanaendelea usiku na kukaukia pale.

Sasa ni sawa kwa housegirl kuifua nguo hiyo?
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger