Waitara Akemea Wanaopuuza Kutimiza Masharti ya Kujikinga na Corona

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Tamisemi,Mwita Waitara leo katika kikao cha kuwapokea wanachama wapya kutoka vyama vya siasa mbalimbali ili kujiuna na Chama cha mapinduzi kwenye  kilichofanyikia ndani ya ukumbi wa CCM  wilaya Tarime amekemea baadhi ya wanasiasa ucharwa wanaotumia nafasi ya ugonjwa wa Corona kupuuza maelekezo yanayotolewa na wizara ya Afya kuhusu kujikinga na ugonjwa huo.

Waitara amesema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa ambao wanatumia nafasi ya ugonjwa uliopo wa Corona kuwaambia baadhi ya watu kupuuza maelekezo yanaypotolewa na wizara ya Afya kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo hatari.

Pia Waitara ametumia nafasi hiyo kuwaonya baadhi ya waendesha vyombo vya moto hususani waendesha pikipiki wa mipakani kama vile mpaka wa Sirari kuwapakia na kuwavusha wageni kutoka Nchi jirani ya Kenya usiku kuingia Tanzania bila kupitia eneo maalumu la mpakani ili kujulikana na kufanyiwa  uchunguzi wa vipimo kama wanamaambukizi ambapo amesema kuwa  vitendo kama hivyo ni hatari kwa kwa maambukizi.

Sasa hivi kuna ugonjwa wa Corona(Cocid19) na serikali imetoa taarifa kwa wananchi wake kujikinga na maambukizi kwa hali hiyo asiwepo mtu wa kupuuza maelekezo ya wataalamu wa Afya kwani kuzingatia kuwa Tarime ipo mpakani mwa nchi jirani ya Kenya na sitokee mwanasiasa anatumia nafasi hiyo kuwapotoshja wananchi na waendesha Bodaboda wanaowapakia watu na kuwavisha mpaka bila kufuata utaratibu wa serikali waache tabia hiyo alisema Waitara.

Kwa upande wake katibu  wa Chama cha mapinduzi wilaya Tarime, Khamisi Mkaruka alisema kuwa leo wamepokea wanachama wapya 55 kutoka vyama vya upionzani  mbalimbali vya siasa wakiongozwa na mwenyekiti wa Chama cha Demokorasia na maendeleo Chadema wilaya Tarime Mwita Joseph.

Kwa upande wake Mwita Joseph wakati akikabidhi kadi ya Chadema kwa Naibu waziri huyo alisema kuwa ameamua kujiunga na CCM ili kumuunga mkono Raisi awamu ya tano Johon Pombe Magufuli kwa kutekeleza shuguli za maendeleo kwa Watanzania na kuwaamini watu wa Tarime na kumteuwa Mwita Waitara kuwa Naibu waziri Tamisemi.

Joseph aliongeza kuwa pamoja nakuunga juhudi za Rais katika kutelekeza shuguli za maendeleo kwa wananchi wake amechoshwa na siasa za Chama alichokuwa Chadema za chuki ambapo alitaja kuwa mwaka 2015 alinusurika kifo baada ya kumwagiwa sumu na wafuasi wa Chama chake cha zamani kisa anaunga aliyekuwa mgombea Ubunge kura za maoni Peter Busene.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad