Hassan Dilunga Kubaki Simba SC kwa Miaka Miwili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa Tanzania bara Simba SC, Hassani Dilunga, amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuendelea kukipiga Msimbazi baada kufikia muafaka mzuri kwa dau la Shilingi Milioni 80.

Kiungo huyo hivi karibuni alikuwa anatajwa kuwepo kwenye mipango ya kusajiliwa na Young Africans kuelekea msimu ujao, ambao wamepanga kusuka kikosi chao.

Dilunga amesaini mkataba huo baada ya ule wa awali wa miaka miwili kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu. Alijiunga na Simba msimu wa 2018/2019 akitokea Mtibwa Sugar ya Manungu mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa zinaeleza kuwa Dilunga alisaini kwa siri yeye pamoja na kiungo mkabaji Said Ndemla wiki mbili zilizopita baada ya kufikia muafaka mzuri kwa pande hizo mbili.

Mtoa taarifa hizo alisema kuwa Simba hivi sasa bado wanaendelea na mazungumzo na baadhi ya wachezaji wengine waliomaliza mikataba yao ya kuichezea timu hiyo inayonolewa na Mbelgiji, Sven Vandenbroeck.

Aliongeza kuwa Dilunga usajili wake ulipitishwa na kocha Sven ambaye amependekeza abakishwe katika kuiboresha safu ya kiungo ya timu hiyo inayoongozwa na Clatous Chama, Francis Kahata na Sharaff Shiboub.

 “Rasmi sasa Dilunga ameongeza mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Simba, hivyo atakuwepo hapa kwa miaka miwili inayofuata ndani ya kikosi chetu cha Simba.”

“Dilunga tangu asaini mkataba ana wiki mbili kwani walisaini pamoja siku moja na Ndemla, hivyo hatakwenda popote pale ikiwemo huko Young Africans ilipokuwa inaelezwa anakwenda.”

“Ilikuwa ngumu kumuachia Dilunga kwenda kwingine kutokana na kiwango kikubwa ambacho amekuwa akikionyesha katika msimu huu, amesaini mkataba kutokana na ubora aliouonyesha Simba,” alisema mtoa taarifa hizi kwa sharti la kutokutajwa jina lake.

 Mtendaji Mkuu wa Simba (C.E.O), Senzo Mazingisa hivi karibuni alitamba kuwabakisha wachezaji wote aliowapendekeza kocha ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu.

“Hakuna mchezaji yeyote atakayeondoka Simba kwa wale wote ambao tunawahitaji labda wale ambao hatuwahitaji ndiyo watakaoondoka,” alisema Mazingisa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad