5/25/2020

Hatimaye Chris Mauki Asimama na Kuwaomba Msamaha Wanaume "Naomba Mniwie Radhi "

Baada ya Chris Mauki Kuwakwanza Wanaume wengi kwa post yake ya leo Instagram, Mwenyewe ameamua kuwaomba msamaha wanaume kwa kupitia post hii hapa chini:

chrismauki_
"Nichukue nafasi hii kwa unyenyekevu sana kueleza maana tarajiwa ya ujumbe wangu ambao umeonekana kuwakwaza wanaume wengi ambao ninauhakika tumetofautiana tu kwenye tafsiri na kama wewe ni mmoja wao unisamehe sana kwa hilo. Mimi pia ni mtafutaji wa chini tu, nimekuzwa kwenye familia ya baba mtafutaji wa kawaida tu kwa hali hii siwezi kamwe kudharau utafutaji wowote wa mwanaume wakitanzania. Nia yangu ilikuwa kuonyesha uhalisi wa baadhi yetu wenye tabia sugu ya kukwepa majukumu ya kuitunza familia kwa kujitetea kuwa sina au sijapata na wakati mke na watoto wanajua sio kweli kuwa baba hana. Baba anaweza kusema sina ila mke na watoto wanaona kunavitu anafanya vinavyoonyesha anahela. Ingawa pia wapo wanaokwepa majukumu yao kwa kudhamiria kabisa. Haya yapo na nyie mnajua ni kweli yapo. Kama kosa ni kutumia neno "msanii" hapo naomba mniwie radhi, sikuwa na nia ovu. Ninakubali kabisa kwamba maranyingine tafsiri ya mmoja inaweza isiwe tafsiri ya mwingine. Amani." Mauki
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger