Mbunge wa CCM aiomba Serikali kufungua chuo cha wizi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mbunge wa Kahama Mjini kupitia CCM Jumanne Kishimba, ameiomba Serikali ifungue chuo cha wizi kwa kuwa matukio ya wizi katika sekta za umma na Halmashauri nyingi umeshamiri kwa kiasi kikubwa na kwamba chuo hicho kitasaidia wale watu wanaoenda kuchunguza wezi, kuzijua mbinu zao na kuwabaini.


Hayo ameyabainisha leo Mei 28, 2020, Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa 19, kikao cha 39, wakati wa uchangiaji wa hoja ya Kamati ya Kudumu ya Huduma za Serikali za Mitaa, na kueleza kuwa ni vyema chuo hicho kikawekwa japo kwa kutumia jina lingine ili kukomesha suala hilo.

"CAG na Waziri wa Fedha yuko hapa hawa vijana wanaoajiriwa lazima wanatoka shule inayofundisha maadili mema na uaminifu, sasa wanaenda kupambana na wizi wengine wamesoma Seminari, kwanini serikali haifikirii sasa kuanzisha chuo cha wizi, kwa maana mtu anapochaguliwa kwa sifa ya uaminifu kwenda kupambana na wezi anaenda kupambana nao namna gani? afadhali apite kwenye chuo hicho kwa miezi mitatu ili ajue akili ya wizi, hawa vijana wetu tutawamalizia magerezani na hali ya wizi ni mbaya sana" amesema Mbunge Kishimba.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad