5/23/2020

Mchumba wa Khashoggi Asema Hakuna Mwenye haki ya Kusamehe Wauaji wake


Mchumba wa Kituruki wa mwanahabari wa Saudi Arabia alieuawa kinyama Jamal Khashoggi, amesema leo kuwa hakuna mwenye haki ya kuwasamehe wauaji wa mwandishi huyo, baada ya watoto wake wa kiume kusema wamewasamehe wauaji.

Khashoggi, mtu wa karibu na familia ya kifalme aliegeuka mkosoaji, aliuawa na kisha mwili wake kutenganishwa katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul nchini Uturuki, Oktoba 2018.

Mrithi wa kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman alituhumiwa kwa kuamuru mauaji hayo, lakini serikali inaendelea kukanusha vikali tuhuma hizo.

Mchumba wake Hatice Cengiz, amesema katika ujumbe wa Twitter, kwamba mauaji ya Khashoggi hayana ukomo wa kisheria na hakuna mwenye haki kusamehe wauaji wake.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger