Shirika la Afya Duniani Lasema Huenda Virusi vya Corona Visiishe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Virusi vya corona huenda ''visiishe''limeonya Shirika la Afya Duniani(WHO)

Akizungumza katika kikao Jumatano, Mkurugenzi wa dharura wa WHO, Dkt Mike Ryan ameonya dhidi ya kujaribu kubashiri ni lini virusi vya corona vitatoweka.

Aliongezakuwa kama chanjo itapatikana, kudhibiti virusi kutahitaji''juhudi kubwa'',

Takribani watu 300,000 kote duniani wameripotiwa kufa kutokana na virusi vya corona, na zaidi ya visa milioni 4.3 vimerekodiwa.

"Ni muhimu kufahamu hili: Virusi vinaweza kuwa janga jingine katika jamii zetu, na , na virusi hivi huenda visiishe ," Dkt Ryan aliwaambia waandishi wa habari kwa njia ya video kutoka Geneva.

"Virusi vya HIV havijaisha - lakini tumevizowea."

Dkt Ryan amesema pia kwamba haamini "mtu yeyote anaweza kubashiri ni lini ugonjwa huu utatoweka ".



Kwa sasa kuna chanjo zaidi ya 100 zainazofanyiwa utafiti- lakini Dkt Ryan amesema kuna magonjwa mengine, kama vile tetekuwanga, ambayo bado hayajatokomezwa licha ya kuwa kuna chanjo yake.

Mkurugenzi Mku wa Tedros Adhanom Ghebreyesus alisisistiza kuwa bado inawezekana kudhibiti virusi vya corona, kwa juhudi.

"Suluhu liko mikononi mwetu, na ni shughuli ya kila mtu, na sote tunapaswa kuchangia kuzuia janga hili ," alisema.
Mtaalamu wa WHO wa majanga Maria van Kerkhove pia ameuambia mkutano wa waandishi wa habari : "Tunapaswa kuweka akilini kwamba itachukua muda kuondokana na janga hili ."

Kauli zao zinakuja huku nchi mbalimbali zikianza kulegeza hatua za kukaa nyumbani, na viongozi wanaangalia uwezekano wa lini na ni vipi wanaweza kufungua shughuli za kiuchumi katika nchi zao.

Dkt Tedros anaonya kuwa hakuna hakikisho juu ya njia za kulegeza hatua za kukaa nyumbani bila kusababisha wimbi jingine la maambukizi.

"Nchi nyingi zingependa kuacha hatua tofauti za kukabiliana na virusi ," alisema mkuu wa WHO . "Lakini pendekezo letu ni kwamba kukaa chonjo kunahitajika bado katika kila nchi kwa kiwangio kiwezekanacho ."

Dkt aliongeza kuwa : " Kuna fikra za ajabu zinazoendelea kwamba sheria ya kukaa nyumbani inasaidia kabisa na kwamba kuondolewa kwake kutakuwa vizuri. Yote yanaweza kusababisha hatari ."
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad