Amber Lulu, Gigy Money Wafika Pabaya


VITA nzito ya mastaa wawili wa kike wa Bongo Fleva; Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ na Gifty Stanford ‘Gigy Money’ imefika pabaya.Sasa kila mmoja anamrushia jiwe mwenzake kwamba ndiye mwenye matatizo, huku wakitoleana matusi ya nguoni.

 Ugomvi wa Amber na Gigy, umekuwa ukifukuta kwa muda mrefu kiasi cha mashabiki wao kuulizana shida ni nini hasa?

Gigy anadai ndiye amempa umaarufu mkubwa Amber, lakini amekuwa akimuonesha dharau.Awali, wasanii hao ambao huko nyuma walikuwa marafiki wakubwa kiasi cha kuishi geto moja na kupiga picha za nusu utupu zilizosambaa kwenye mitandao mbalimbali na kuwafanya wajulikane, walikuwa marafiki wakubwa mno.

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA linafahamu kuwa, baada ya kila mmoja kurekodiwa video na kupigwa picha za utupu kisha kusambaa mitandaoni, wawili hao walianza kuwa maarufu ambapo Gigy alipata shavu la kutangaza kwenye Televisheni ya EATV.

Baadaye Gigy alijikita kwenye muziki ambapo Amber naye alimfuata hukohuko ndipo bifu lilipoanza rasmi.Lakini pamoja na mambo mengi yanayosemwa, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA linafahamu kuwa, chanzo cha vita ya Amber na Gigy ni kuibiana madanga (mabwana).

 “Unajua wote wawili walikuwa na ndoto za kuwa mastaa.“Kila mmoja alitafuta njia ya kutoka, sasa bifu likaanza walipoamua kuingia kwenye muziki, ikawa ni shida na malumbano na mpaka sasa wanatoleana siri zao za ndani hadi kwenye mitandao ya kijamii,” anasema rafiki yao wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina.


IJUMAA WIKIENDA limekuwa likimchimba Amber juu ya tatizo ni nini kati yake na Gigy, ambapo alisema;“Mimi ninamshangaa sana mwenzangu, sijawahi kumkosea, akiwa na jambo lake lolote, lazima nishirikiane naye, lakini kwenye jambo langu hajawahi kushirikiana na mimi.

“Yeye ameendelea kufanya kazi ya kunishutumu kila siku bila sababu.”Amber aliongeza kuwa, Gigy amekuwa akisema kwamba, yeye ndiye aliyempa umaarufu, jambo ambalo siyo kweli kwani yeye alipata jina baada ya video yake ya utupu kuvuja.

“Mimi nimetoka Mbeya mwenyewe, sijaletwa na mtu hapa Dar na hata anavyosema kuwa amenileta Dar na kunipa umaarufu, siyo kweli, maana nilijulikana kwa video yangu ya utupu iliyovuja, hivyo aache kunisema kwani sijawahi kumkosea chochote.

 
“Hata mkimuita yeye na mimi ili aulizwe ana shida gani na mimi aseme nitakuwa huru sana, lakini siyo kuendelea kunisakama kila kukicha,” anasema Amber akionesha kuchukizwa na kinachoendelea kati yake na Gigy.

Kwa upande wake, Gigy alipotafutwa na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, alisema hana muda wa kumzungumzia Amber kwa sababu ana vitu vingi vya maana vya kufanya.“Niko bize na vitu kibao, sina muda wa kumuongelea Amber, nina vitu vya maana vya kufanya,” anasema Gigy.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments