6/18/2020

Bulembo "Unachukuaje Fomu ya URAIS Wakati Magufuli Hajamaliza Vipindi vyake Viwili?"Aliyekuwa Mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo, amesema taratibu haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea Urais zaidi ya John Magufuli

Amefafanua, “Kwa mujibu wa sheria kama wewe ni mwana-CCM, Rais anatakiwa awe katika vipindi viwili sasa unatokea wapi kuchukua fomu? Unajadiliwa kikao gani?"

Bulembo amesema hataki kugombea (Ubunge) licha ya kwamba anajua atashinda na kwamba haiwezekani nyumba nzima wawe Wabunge

Ameongeza, “Nataka niondoke salama, mtoto wangu Halima yupo kwenye jimbo, mke wangu naye yupo kwenye jimbo anagombea Viti maalum, haiwezekani nyumba yote kuwa Wabunge haileti picha nzuri"

Aidha, amesema “Nimejifunza vingi tangu nimeteuliwa na Rais, wenzetu wanaoendelea kutafuta majimbo wanaendelea kugombea, juzi Rais alivyosema kwa herini kila Mtu ameshakwenda kwenye jimbo lake, bado nipo Dodoma napumzika, niko kwenye kustaafu, sina presha sina haraka ya kwenda popote"
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger