Calisah Afikishwa polisi, Amber Lulu Ahusika


Mwanamtindo Calisah anadaiwa kufikishwa kituo cha polisi cha Urafiki na kutolewa dhamana na msanii Amber Lulu kwa kosa la kurudisha gari aina ya Vitz ambalo alikuwa amekodi likiwa lina matatizo ya vioo vya pembeni, mafuta na kushindwa kulipia pesa.


Akizungumza na EATV & EA Radio Digital mwenye kesi hiyo aitwaye Edger ameeleza kuwa "Aliniomba nimkodishie gari kwa siku tatu, tukakubaliana kila siku ni elfu 50 yeye alinilipa elfu 60 tu baada ya laki na nusu, akalirudisha gari halina mafuta, ameigonga vioo vya pembeni "side mirror", ameiua monitor bila ya kuniambia na akani-block kwenye simu, nikamshtaki polisi kwa kuniharibia vitu vyangu venye thamani ya laki mbili na 60" 
"Bahati nzuri nikampigia simu mshakaji wake Amber Lulu akamsaidia kutoa Laki moja na nusu, hela bado hajanimalizia hadi sasa hivi bado namdai" ameongeza.
Kwa upande wa mtuhumiwa Calisah amesema "Sio kweli Sijawahi kukamatwa na polisi tangu mwaka huu uanze hizo ni stori za kizushi puuzieni, hao watu wanatafuta umaarufu ukishajua unajulikana kuna vitu vingi sana vinatokea na mimi nafahamika sana" That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments