Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Gundu la Kumwacha Mume wa Ndoa Laniandama..Niliekimbilia Kwake Kanitelekezea Watoto Wake Wawili

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Mimi ni Mama wa watoto wawili, nilikua nimeolewa lakini niliachana na mume wangu baada ya kumpata mwanaume mwingine. Mume wangu ni mfanyabishara wa kawaida, lakini kuna kipindi nilikutana na Kaka mmoja ambaye ni injinia, alikua akijenga jingo flani hapa mjini na alikua ni rafiki wa rafiki wa mume wangu. Alinitongoza tukaanza , mahusiano ya siri ila baadaye penzi lilikolea. Yeye alikua na mwanamke ambaye ni mke wa ndoa, baada ya sisi kupendana alimuacha mke wake, akampa talaka na mwanamke akaondoka akaacha watoto wawili.

Alipoachana na mke wake na mimi nilidai talaka kwa mume wangu tukanza kuishi pamoja kama mke na mume ingawa hatukufunga ndoa. Kwani bado alikua hajanitambulisha kwao. Maisha yalikua mazuri, lakini tatizo nikuwa mwaka jana yule Kaka alikamatwa na polisi, kuna pesa walimuibia muajiri wao, alipokamatwa alikaa ndani kama kwa mwezi mmoja hivi nikawa mimi ndiyo nahudumia familia. Alikuja kutoka. Lakini alipotoka alikua hana kazi tena ingwa kesi bosi wao hakutaka kuendelea nayo.

Hapo ndipo mambo yalibadilika, alianza kunipiga, kunitukana na kuniambia kuwa mimi ndiyo nina gundu na nina kisirani kwakua nimeanza kuishi naye nikapata mabalaa. Nilivumilia kwani sikua na pakwenda, wakati huo nilikua na ujauzito na sikua na kazi. Mwaka huu mwezi wa tatu aliniambia kuwa kuna kazi kapata huko Kigoma anaenda kwani alikaa muda bila kazi, sikua na namna, alienda na kuniachia wanae wawili ukichanganya na wakwangu basi wane.

Lakini Kaka mpaka sasa mwanaume hajarudi, alipoondoka tu ndiyo kimoja, hapatikani kwenye simu na wala sijui anafanya kazi wapi. sifahamu ndugu yake hata mmoja na mke wake wa zamani sijui yuko wapi, nimechanganyikiwa sina kazi, mume wangu wa zamani baada ya kuona wanae wanateseka alikuja na kuwachukua kinguvu hivyo hatoi matumizi tena, pesa ya matumizi aliyokua ananipa X wangu ndiyo nilikua nahudumia watoto ila sasa sina kitu nahangaika na wanae wadogo hata kwao sipajui kusema niwapeleke naomba ushauri wako Kaka nifanye nini kwani nimechoka na hi hali na sijui chakufanya.

Post a Comment

0 Comments