Nyani Afungwa Kifungo Cha Maisha Kwa Mauaji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Dunia ina mambo unaambiwa tembea ujionee, pengine hii ni kutokana na matukio kwenye maeneo mbalimbali tofauti na eneo ulilipo kwa sasa.

Katika hali isiyo ya kawaida huko nchini India mnyama aina ya Nyani amehukumiwa kufungwa kwenye chumba cha pekee kwenye kipindi chote cha maisha yake kutokana na vitendo vya uhalifu.

Mbali na vitendo vya kihalifu imedaiwa Nyani huyo kusababisha kifo.

Imedaiwa kuwa nyani huyo ameshajeruhi watu 250 katika mji wa Mirzapur nchini India na mtu mmoja kati ya wahanga wa kuvamiwa amefariki kutokana na majeruhi aliyoyapata.

Inadaiwa kuwa  Nyani huyo alianza tabia za ukorofi baada ya mmliki wake aliyekuwa mwanamazingaumbe kufariki dunia miezi kadhaa iliyopita .

Nyani huyo alianza kuwa mwenye hasira na kuwarushia watu mawe na kuvamia watoto na kina mama anapopata nafasi.

Wataalamu wa maswala ya wanyama walifanikiwa kumtia nguvuni nyani huyo na kubaini kuwa kinachomfanya awe mwenye hasira ni kukosa kinywaji ambacho alikuwa anapewa na mmiliki wake wa awali.

Baada ya uchunguzi wa kina wataalam waliamuru nyani huyo kufungwa kwenye chumba maalum ili asilete madhara zaidi kwa binadamu hata wanyama wenzie.

CHANZO: Efm Tanzania (Instagram)
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad