Umoja wa Afrika waunga mkono pendekezo la Rais Magufuli
Umoja wa Afrika (AU) imerudia wito wake wa kuzitaka taasisi za fedha za kimataifa kuzifutia madeni nchi za Afrika, na kutekeleza mpango wa kuziwezesha nchi hizo kukabilia na janga la virusi vya corona.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni za Benki ya Dunia (WB) kwa jumla, nchi za Afrika zinadaiwa dola bilioni 493.6 (shilingi quadrilioni 1.14).

 

Kauli za viongozi hao zimekuja ikiwa baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kuzitaka taasisi za fedha za kimataifa kuzisamehe madeni nchi za Afrika badala ya kuzikopesha fedha ili ziweze kukabiliana na corona.

“Badala ya kutoa ofa ya kukopesha tena kwa ajili ya kupambana na corona wasamehe madeni walizozikopesha hizi nchi. Wakisamehe madeni, mapato ya hizi nchi yatatumika kupambana na corona,”- alisema Rais Magufuli Aprili mwaka huu akizungumza wilayani Chato.

Mnamo Aprili mwaka huu WB ilisema kwamba nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara mwaka huu zitashuhudia kushuka kwa uchumi ambako hakujawahi kutokea kwa miaka 25, ikiwa ni athari za janga la corona.

Hata hivyo Rais Magufuli alisema kuwa kutokana na hatua ambazo Tanzania imechukua uchumi wake utashukua na kukua kwa asilimia 5.5.

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne baada ya mkutano kwa njia ya mtandaoni wa wakuu wa nchi wanachama wa AU na ujumbe maalum, viongozi hao pia walitaka kuondoa vikwazo dhidi ya Sudan na Zimbabwe ili kuwezesha nchi hizo mbili kukabiliana kikamilifu shida kuzorota kwa huduma za afya dunia.

Jumla ya visa zaidi ya 200,00 vimethibitishwa barani Afrika ambapo kati ya hivyo asilimia 61 ni kutoka Algeria, Afrika Kusini, Nigeria, Misri na Ghana.


That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments