6/21/2020

Vanessa Mdee aeleza sababu za kuachana na muziki Rotimi ahusishwa ‘Muziki ni pepo, kwa sasa naishi Marekani’Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Vanessa Mdee ambaye alikuwa anaunda ametangaza kuachana na muziki wa Bongo Fleva kupitia Podcast yake aliyopost aliyoipa jina la “Deep Dive With Vanessa Mdee”Kupitia Podcast hiyo Vanessa Mdee ameeleza mambo mengi sana aliyopita kwenye muziki wa bongo Fleva hadi kufikia hapa alipo kwa sasa, Kupitia Audio hiyo alifikia wakati akisema muziki wa Bongo Fleva ni demonic akimaanisha muziki ni Pepo.

Mbali ya kuzungumzia kuachana na muziki Vanessa pia ameeleza alivyopitia wakati mgumu hadi kujiingiza kwenye ulevi wa pombe kisa muziki lakini pia alipishana kauli na mama yake baada ya kujiingiza kwenye muziki, akiongeza kuwa mama yake ni mtu wa dini hivyo aliamini mwanae kama anapotea hivi kutokana na kile alichokuwa akifanya Vanessa yaani muziki.

Kupitia kwenye Podcast hiyo hii ni moja ya sehemu aliyoizungumzia:-

“Nafahamu nitawakwaza watu wachache ila ni sawa tu, Najua mashabiki zangu hawataki kusikia hili lakini hebu vuta picha, sipo mbali sana na nyie, Sababu za kwanini nimeamua kuachana na muziki ni kwa sababu ninahitaji kuchagua maisha yangu, huu muziki ni pepo (demonic) Wapo wengi watakwambia nusu ya ukweli kuhusu ukweli wa kinachoendelea kwenye hii tasnia, na ukweli ni kwamba ninataka kuwa wakili mzuri wa uaminifu na ukweli na kuwa wakili mtiifu, Kuamua kuachana na kitu ambacho umekuwa ukikifanya kwa muda mrefu na kwa juhudi juhudi,

Vanessa aliongeza kuwa Sitaki kuwa kama Pipi ambayo juu imepambwa kwa nakshi nzuri za kuvutia lakini ukiifungua unakutana na kitu tofauti, Najua wengi watajiuliza kuhusu hiki kwamba hivi Vnessa hataimba tena, au hatutakuona tena ukitumbuiza na kufanya muziki, Kiukweli mimi Napenda muziki, napenda kutumbuiza, hiki ndicho  kitu ambacho nimeletwa kukifanya duniani, Ukweli ni kwamba labda nililetwa kupitia hii tasnia ili nije nikusimulie kwa uaminifu, ukweli kuhusu vitu ambavyo huwezi kuambiwa sehemu yoyote” Hapa alikuwa akimaanisha ukweli na yanayofanyika kwenye huu muziki ambao yeye aliuita kuwa ni demonic yaani Pepo.

Lakini Vanessa hakusita kumtaja mpenzi wake Rotimi kuwa ni mmoja ya watu ambao wamemukoa sana katika hali ambayo alikuwa anapitia kabla ya kukutana nae.

Mambo mengi sana amesimualia Vanessa mdee hasa yale yanayosikitisha kuhusu tasnia ya muziki aukweli wake lakini pia hali ngumu aliyopitia kwenye maisha ya muziki, Lakini Vanessa alimaliza kwa kusema kuwa kwa sasa anaishi nchini Marekani na mpenzi wake Rotimi katika mjengo ambao mpenzi wake huyo ameununua huko Marekani.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger