Aliyekuwa Kocha wa YANGA Akutana na Rungu Jingine, Afutiwa Vibali Afrika Kusini


Shirikisho la Soka la nchini Afrika Kusini (SAFA) limemfutia jumla vibali vya kazi Luc Eymael aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga kufanya kazi ndani ya nchi hiyo. Imeeleza taarifa kupitia tovuti ya SAFA.

Itakumbukwa, Eymael Julai 26 baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli alisambaza taarifa ambazo zilikuwa zinaonyesha ubaguzi wa rangi na kusema watanzania hawajui soka.

Tayari Yanga imeshamfuta kazi Eymael jumla kutokana na kitendo hicho na kuomba radhi kwa mashabiki, Serikali na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).

Kocha huyo pia aliomba msamaha kwa kueleza kuwa alifanya hivyo kutokana na hasira alizokuwa nazo kwa kupitia kipindi kigumu ndani ya Yanga.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments