7/31/2020

Bernard Morrison "Kukamatwa Kwangu ni Njama za Yanga "


NYOTA raia wa Ghana, Bernard Morrison ameingia katika sekeseke jingine baada ya kukamatwa na kushikiliwa kwa muda na Polisi wa Kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Morrison alishikiliwa na Polisi ambao waliisimamisha gari aliyokuwa amekodi ya Uber na kumuambia wamesikia harufu ya bangi.

Kwa mujibu wa mashuhuda, walieleza Morrison akiwa na dereva wa Uber aliwaruhusu askari hao kuanza kupekua kama kweli wameona au wataona bangi, lakini haikuwa hivyo.“

Baadaye wakasema kwamba wanataka simu ya Morrison, jamaa akagoma kuitoa na ku-charuka sana akisema hawezi kuwapa na wako tayari wampe-leka Polisi.

Basi ukaibuka mzozo na dereva wa Uber akaanza kuwaamua akiwasisitiza kwamba kama wamehisi kuna bangi kwenye gari wakague kwa kuwa yeye havuti “jani” na wala mteja wake haku-fanya hivyo.“

Basi wale askari wasisitiza walitaka simu ya Morrison, baadaye wakawachukua wakisema wanawapeleka Kituo cha Oysterbay huku Morrison akisema watu wa Yanga ndiyo wanamfanyia vile,” kilieleza chanzo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger