7/25/2020

Bosi Simba: Usajili Wetu Utakuwa wa Balaa!


Mmipango mizito ya usajili ambayo inayofanywa na mabosi wa Simba wakiongozwa na mwekezaji wao Mohammed Dewji ‘Mo’ imebainika kwamba kikosi hicho hakitakuwa na namba kubwa ya wachezaji wapya watakaosajiliwa.

Mabosi hao wa Simba wamepanga kuwa na kikosi cha wachezaji 28 pekee kwa ajili ya kuongeza ushindani wa namba na kutwaa mataji miongoni mwa wachezaji hao.

Kikosi hicho kitaundwa na wale ambao watabakia mwishoni mwa msimu na wale wapya ambao watasajili katika dirisha kubwa la usajili ambalo huenda likaanza Agosti, mwaka huu.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa raia wa Afrika Kusini ameliambia Championi Ijumaa, kuwa kwenye kikosi hicho cha msimu ujao kitakuwa na wachezaji wachache kwa kutotaka nyota wao kutozembea badala yake wawe na ushindani wa namba.

“Hatuwezi kuwa na kikosi cha wachezaji zaidi ya 30 badala yake tutakuwa na kikosi cha watu wachache kwa ajili ya kuwafanya wainjoi mpira.


“Lakini pia tunataka kuona wanashindana juu ya nafasi za kucheza na hilo ndiyo lengo letu. Tutasajili wapya na kuacha wachezaji kwa msimu ujao lakini hawatazidi namba hiyo ambayo tunaitaka,” alimaliza Msauz huyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger