Ticker

6/recent/ticker-posts
.

CCM Yampongeza Hamisa Mobeto!

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Mazito yamemfika msanii wa Bongo Fleva, mwanamitindo Hamisa Mobeto baada ya hivi karibuni kuonesha anauza vitenge vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mobeto alipata tenda hiyo ya kuuza vitenge vya CCM ambavyo vimemzulia balaa.

Baada ya kupokea tenda hiyo na kuposti mtandaoni, yakaibuka maneno kutoka kwa mashabiki wasiomtakia mema, japo wengine walimuunga mkono kwa kupata kazi hiyo kubwa.

“Jamani Hamisa anajua kutumia fursa mpaka raha maana anapambana sana, anachakarika huku na kule kuhakikisha anapata pesa siyo kama wasanii wengine wanaowaza kudanga na kwenda Dubai kuendesha mapikipiki.

“Hamisa anajielewa na atauza vitenge mpaka awe kama Bilionea Laizer, Mungu amjalie aweze kufikia malengo yake,” alisema mmoja wa wafuasi wake kwenye ukurasa wake wa Instagram anayejiita Wittie.
 
Mbali na kusifiwa, mashabiki wengine walionesha chuki zao binafsi kutokana na Mobeto kupata tenda hiyo kwa kusema kuwa, hawezi mambo ya siasa aendelee na mambo yake ya kudanga.

“Huyu dada na CCM wapi na wapi, mbona kama anatafuta pa kuchuna au madanga yamemuishia? Mbona mwaka huu tutajionea mengi?“Unajua nilipoona kaposti vitenge vya CCM nilicheka kwa sauti, yeye aendelee na kazi yake ya sanaa na kudanga ila kwenye mambo ya siasa awaachie wenye siasa zao,” alisema shabiki mwingine.

Baada ya mambo kuwa mengi mtandaoni, Gazeti la IJUMAA lilimvutia waya Mobeto ili aweze kuzungumzia kuhusiana na ishu ya kushambuliwa mtandaoni ambapo alisema kuwa hawezi kuzuia kusemwa. “Acha waseme tu, mimi siwezi kuwazuia watu kusema kwani mpaka kufikia hapa nimesemwa mangapi…”

Stori: Khadija Bakari, Ijumaa

Post a Comment

0 Comments