Ticker

6/recent/ticker-posts
.

RC Songwe Awatandika Viboko Wanafunzi Waliohusika Kuchoma Shule

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amewachapa viboko wanafunzi watano waliohusika katika tukio la kuchoma moto shule ya sekondari ya Wavulana ya Oswe na kusababisha hasara ya Zaidi ya Tsh. Milioni 26.

Brig. Jen. Mwangela amefikia hatua hiyo mara baada ya kamati aliyoiunda ya kuchunguza chanzo cha ajali ya moto uliotokea shuleni hapo Julai 3 mwaka huu kubaini kuwa wanafunzi wawili Naftari Nganga na Collin Kisinga ndio waliochoma mabweni ya shule hiyo huku wenzao watatu wakiwa na taarifa za mipango hiyo na hawakuripoti.

Amesema wanafunzi hao walianza mpango wa kuchoma moto mabweni mnamo Juni 28 kwa kununua vifaa vya kuchomea, ilipofika Julai 2 walijaribu kuchoma bweni lakini halikuwaka, Julai 3 walichoma bweni likawaka na kusababisha hasara hiyo na Julai 6 walifanya jaribio lingine tena la kuchoma moto ghala la chakula lakini halikuwaka moto.

Brig. Jen. Mwangela ametoa miezi mitatu kwa Wazazi wa Naftari na Collin kila mmoja alipe shilingi Nilioni 7.3, Mmiliki wa Shule pia alibainika kuwa na uzembe wa kuweka vifaa vya kuzimia moto hivyo ameagizwa alipie Tsh. Milioni 7.3 huku Mwalimu wa zamu siku ya tukio, mlinzi na Patroni nao wakitakiwa kulipa Tsh. Milioni 4 ili kufidia hasara iliyotokana na ajali hiyo ya moto.

Post a Comment

0 Comments