7/12/2020

Jack Wolper "Sintaweza Kuja Kumsahau Dallas Yule Ndo Mwanaume"

Licha ya kuwa ana mke kwasasa, Pichani Dallas aliyewahi kuwa mpenzi wa Wolper 2012 kwenye interview mpya na Globalpublishers anasema hajaona mwanamke mwingine wa kumpenda kwenye maisha yake yote yaliyobaki duniani zaidi ya Jacqueline Wolper

.“Huyu ndiye mwanamke wa maisha yangu. Hilo litaendelea kuishi kwenye maisha yangu hadi mwisho wa uhai wangu. Ninampenda sana Wolper na nitaendelea kumpenda siku zote,” anasema Dallas ambaye baada ya uchumba wake na Wolper kuvunjika, alioa mwanamke mwingine na bado yupo naye.

Aliongeza kuwa, ikitokea akapata pesa tena kama kipindi kile, basi mtu ambaye atamuoa tena kwa harusi kubwa ni Wolper.

“Nakwambia mimi nikibahatika kupata pesa kama kipindi kile, kazi yangu itakuwa ni moja tu, kumuoa Wolper, sijaona mwanamke mwingine kwenye maisha yangu.” anasema Dallas huku akiinua mikono juu kumuomba Mungu amsikilize dua yake.

“Sina tatizo kabisa na Dallas na tunapendana mno, tunapiga stori na akiwa na kitu chochote lazima anakuja pale dukani kwangu (Sinza-Makaburini, Dar) tunaongea. Hata kanzu na kofia huwa ninamnunulia mimi, sisi siyo maadui, ni marafiki wakubwa sana,” Wolper ameiambia Globalpublishers
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger