7/14/2020

Jambazi Sugu Aliyehusishwa na Mafia Marekani Afariki kwa njia ya Kushangaza Gerezani

Jambazi sugu aliyehusishwa na Mafia Marekani afariki kwa njia ya kushangaza gerezani

Jambazi huyo mwenye umri wa miaka 89 alifikishwa katika hospitali ya gereza hilo akiwa tayari ameaga dunia muda mfupi baada ya kuhamishwa kutoka jela la Florida.

Afisa wa muungano wa magereza ameliiambia shirika la habari la Associated Press kwamba kifo chake kinachunguzwa kama mauaji.

Maisha ya Bulger, ambaye alifungwa mwaka 2013 baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya watu 11, yaliangaziwa katika filamu kadhaa.

Kiongozi huyo wa zamani wa genge la majambazi wa mji wa Winter Hill kusini mwa Boston aliangaziwa katika filamu ya Black Mass iliyoigizwa na Johnny Depp, na The Departed, ambazo zilishinda tuzo ya Academy kwa picha bora mwaka 2007.

Kifo chake kilitokea siku ambayo alihamishwa katika gereza la Hazelton lililopo West Virginia, ambalo lina wafungwa takribani 1,385.

Vyanzo tofauti vya habari vimeiambia Boston Globe kuwa mfungwa mmoja anayedaiwa kuwa na uhusiano na mafia anachunguzwa kuhusiana na mauaji ya Bulger.

Inasadikiwa kuwa Bulger alishambuliwa vibaya na wafungwa wenzake muda mfupi baada ya kufikishwa katika gereza hilo.

Kwa mujibu wa runinga ya WFXT-TV,mjini Boston, Bulger aliuawa saa kadhaa baada ya kujumishwa na wafungwa wengine.

Wiki iliyopita maafisa wa magereza walikataa kutoa tamko lolote kuhusu hatua ya kumhamisha Bulger ambaye anahudumu kifungo cha maisha katika jela la Florida .

Lakini kwa mujibu wa Globe, Bulger alihamishiwa jela la Florida mwaka 2014 kutoka jela nyingine mjini Arizona baada ya uhusiano wake namshauri wake wa kike kuvutia mamlaka ya magereza.

Maelezo kuhusiana na kifo chake hayajatolewa lakini, maafisa wa magereza wameithibitishia shirika la habari la CBS kwamba kuna tukio la "mauaji" lilitokea Jumanne asubuhi.

"Haya ni mauaji ya tatu katika kipindi cha miezi saba katika gereza hili," Richard Heldreth alisema katika mahojiano ya simu."

Taarifa iliyotolewa na idara ya magereza siku ya Jumanne imethibitisha kifo chake akiwa gerezani custody, na kuongeza kuwa shirika la upelelezi la Marekani,FBI, limeanzisha uchunguzi.

James 'Whitey' Bulger ni nani?

Bulger alizaliwa mwaka 1929 katika familia ya wamarekani wenye asili ya Ireland.

Alilelewa katika kanisa la wakatoliki wa Ireland mjni Boston, ambako alijiunga na genge la Shamrocks, alianza kwa kuiba magari na baadaye akapanda daraja kwa kuingia kaka uhalifu wa kuiba katika benki.


Mara ya kwanza alikamatwa kama kama mhalifu mdogo na hatimaye aliendelea kutawala mamlaka ya uhalifu, kama vile kamari, ulaghai, kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na mauaji.

Baada ya kushtakiwa na kuufungwa kwa kosa la wizi wa mabavu na utekaji nyara alipelekwa katika jela masarufu la Alcatraz katika kisiwa cha San Francisco

Inasemekana aliipenda jela hilo sana kiasi cha kuitembelea akijidai kuwa mtalii wakati alipokua mafichoni.Aliwahi kuwanyonga wanawake wawili kwa kutumia mikono yake na pia kumtesa mwanamume mmoja kwa saa kadhaa kabla ya kumiminia risasi ya kichwa na kumuua

Je majambazi hawa ndio wajinga zaidi Duniani?
Inasemekana Bulger hakulipenda jina la utani la Whitey - ambalo lilinatokana na nywele zake nyeupe. Alipendelea kutambuliwa kwa jina la Jimmy.

Shughuli zake za kijambazi ziliimarishwa na maajenti wa wabaya wa FBI ambao walimtumia kupata taarifa kuhusiana na magenge mengine ya uhalifu.


William kaka yake Bulger alikuwa mwanasiasa maarufu wa chama cha Democratic na hatimaye alichaguliwa kiongozi wa wa bunge la seneti kutoka jimbo Massachusetts mwaka 1978 na baadaye rais wa chuo kikuu Massachusetts.

Mwanasiasa huyo alikanusha madai ya kuwa na ufahamukwamba ndugu yake ni mhalifu, lakini baadaye alikiri kuwa anampenda sana ndugu yake na kamwe hawezi kumsaliti

Bulger alikimbilia mafichoni mwaka 1995 baada ya mmoja wa majenti wa FBI kumdokezea kwamba kuna mpango wa kumkamata.

Jambazi huyo sugu alikamatwa mwaka 2011 katika eneo la Santa Monica, California, ambako amekuwa akjificha akiwa na mpenzi wake Catherine Greig.

Bulger alihukumiwa ifungo gerezani mwaka 2013 baada ya kupatikana na msururu wa makoso ya uhalifu, ikiwa ni pamoja na mauaji 11 katika miji tofauti nchini Marekani katika miaka ya 1970 na 1980.

Serikali ya Marekani iliwalipa wahasiriwa waake fidia ya dola milioni 20 kwa misingi kwamba alitekeleza mauaji hayo chini ya uangalizi wa serikali

Mwaka 2015 kundi la wanafunzi lilitumia somo la historia kumuandikia waraka wa kumtaka aachane na mienendo yake mibaya.

Bulger alionekana kuguswa na waraka huo ambao ulimfanya kuonekana kujutia maisha yake ya zamani aliposema,

"Maisha yangu yameharibika kwa kuishi kipumbavu,"
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger