Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Lulu "Kupigwa na ugomvi tu Ndio ulizaa Tatizo Kubwa Lililobadili Maisha Yangu kwa Sekunde tu na Kuishia Kala"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Lulu "Kupigwa na ugomvi tu Ndio ulizaa Tatizo Kubwa Lililobadili Maisha Yangu kwa Sekunde tu na Kuishia Kala"

WAKATI bado kukiwa na mjadala mzito juu ya kipigo alichokipata staa wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kutoka kwa mumewe Ashraf Uchebe, staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka jinsi kipigo cha aliyekuwa mwandani wake marehemu Steven Kanumba kilivyobadili maisha yake.

Akizungumza kwenye Insta Live kwenye ukurasa wake wa Instagram, Lulu alisema kuwa kipigo cha Kanumba kilibadili maisha yake kwa dakika chache tu na kusababisha kwenda gerezani.

“Pengine watu mnasahau, kitu kilichofanya niende gerezani ni kupigwa, ugomvi tu ambao ulizaa tatizo kubwa lililobadili maisha yangu kwa sekunde tu.

“Ni kitu ambacho nimekipitia, najua madhara yake na jinsi kilivyonibadili, hivyo hata ikitokea kwa sasa siwezi kuvumilia kabisa.

“Kwa namna yoyote hata ni-date na Bill Gates nikaona kuna namna napigwa, siwezi kuvumilia,’’ amesema Lulu.

Tukio hilo lililotokea Aprili 7, 2012 nyumbani kwa marehemu Kanumba maeneo ya Sinza- Vatican jijini Dar ambapo wapenzi hao walikuwa na ugomvi wa kawaida.

Siku ya tukio Lulu alikiri kuwa alipigwa na Kanumba kiasi kwamba alipopata upenyo alimsukuma na kusababisha Kanumba kuteleza na kuanguka na ndiyo sababu ya kupoteza uhai wake na Lulu kwenda jela.

Mbali na hilo, Lulu aliwavaa wanaomsema anapigwa na mchumba’ke wa sasa, Francis Ciza (DJ Majizzo) na kusema kuwa hajawahi kumfanyia ukatili wa namna hiyo.

“Sijui nani alianzisha hii stori na sijui ilianza vipi, mchumba wangu hajawahi kunipiga hata kunitia singi.

“Hajawahi kunifanyia ukatili wa kijinsia kwa namna yoyote, sikutaka kuzungumzia kwa sababu saa nyingine mtu anaweza kukuchokonoa ili apate ambacho kipo.

“Mara nyingi huwa sitoi hiyo nafasi, ndiyo maana muda mwingi naweza kuongelea na kutania ili watu wacheke au nicheke.

“Sasa nikaona ni tuhuma ambayo inakaa muda mrefu na huu ni mwaka wa tatu vitu vinaendelea kila siku na hii si tuhuma nzuri.

“Juzi ilivyotokea kwa Shilole, nikaenda kukomenti watu wakaanza kusema na wewe ongea tunasikia unapigwa.

“Yaani mtu anaongea utasema ana uhakika na chanzo chake cha habari.

“Watu wanasema navumilia kwa sababu kuna hela, sawa hela zipo ila siwezi kupoteza utu wangu, kupoteza kujiamini kwangu, hata ingetokea nisingeweza kuvumilia ukatili.

“Tangu nimekuwa kwenye uhusiano na mchumba wangu ni mwaka wa tano tunakwenda wa sita, mtakuwa mashahidi watu wengi wamekuwa katika uhusiano tofauti tofauti,’’ alisema Lulu na kufunga mjadala huo.


Post a Comment

0 Comments