Timu ya Fenerbahce ya Uturuki Yamtaka Mbwana Samatta

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kwa mujibu wa gazeti la habari za michezo la Nchini Uturuki la Takvim limeripoti kuwa klabu ya Fenerbahce ya Uturuki inavutiwa na mshambuliaji mpya wa Aston Villa ya England, Mbwana Samatta.

Mshambuliaji huyo raia wa Tanzania alijiunga na Villa katika dirisha la usajili lililopita akiwa chaguo la kwanza ili kuziba pengo la Mbrazil, Wesley aliyekuwa akisumbuliwa na majeraha.


GENK, BELGIUM – AUGUST 22 : Ally Mbwana Samatta forward of KRC Genk, Philippe Clement head coach of KRC Genk during a press conference before the UEFA Europa League Play-Offs 1st Leg match between KRC Genk and Brondby IF on August 22, 2018 in Genk, Belgium, 22/08/2018 ( Photo by Vincent Kalut / Photonews
via Getty Images)

Samatta ameshindwa kuleta mafanikio ndani ya Aston Villa katika michezo yake ya Premier League baada ya kufunga goli moja 1  pekee katika michezo 12 aliyocheza.

Kwa mujibu wa Takvim, Fenerbahce inakaribia kumnasa Samatta kutokana na hali iliyopo kwa sasa ndani ya Aston Villa na itawakilisha ofa yake ya kumchukua kwa mkopo kutoka katika klabu hiyo ya Birmingham.

Inadaiwa yapo makubaliano ya maneno baina ya Samatta na Villa kuwa Aston Villa itatakiwa kumruhusu kujiunga na klabu nyingine endapo timu hiyo haitafanikiwa kuwepo Premier League katika msimu ujao.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad