7/26/2020

Mama Nandy "Sipendi Nandy Aingie Kwenye Ndoa"


MAMA mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Fausta Mfinanga, maarufu kama Nandy, ameweka bayana juu ya maamuzi ya mwanaye kufunga ndoa na msanii mwenzake, Bill Nas, ambaye ni mpenzi wake wa muda mrefu sasa.

Akizungumza na Global TV wakati wa uzinduzi wa Nandy Bridal, mama Nandy amesema; “Siwezi kusema tumemkubali Bill Nas au tumemkataa, Nandy ni mtu mzima anachokifanya anakijua, kwa hiyo hatuwezi kumchagulia aolewe na nani, ni uhuru wake kuchagua.

“Lakini kwa sasa nisingependelea aingie kwenye mambo ya ndoa kwa sababu ana malengo yake, ana vitu vyake anavyotaka kuvifanya ili afikie mafanikio yake, kwa hiyo mimi naona angefanya kwanza kazi yake, haya mengine yatakuja,” amesema Mama Nandy.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger